HabariNews

Mahakama ya Embu yaondoa marufuku ya Muguka Mombasa, Kilifi na Taita taveta kwa muda.

Mahakama kuu  ya  Embu imetoa agizo la kusitishwa kwa utekelezwaji wa marufuku dhidi ya mugukaa katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Taita Taveta hadi kesi iliyowasilishwa isikilizwe na kuamuliwa.

Jaji Lucy Nyuguna katika alitoa uamuzi huo mnamo siku ya Jumanne Mei 28, akiitaja kesi inayopinga  iliyowasilishwa na bunge la kaunti ya Embu na Chama cha Ushirika cha Muguka cha Kutherema kama ya dharura, akiongeza kwamba agizo hilo linafaa kufuatawa na litabakia hadi Julai 8 mwaka huu.

Mahakama hiyo kadhalika ilitoa agizo kwamba ombi hilo liwasilishwa kwa washtakiwa katika kipindi cha wiki Moja.

“ Inaposubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi hili, agizo limetolewa kuzuia/ kusimamisha washtakiwa na Ma-agenti wao dhidi ya kutekeleza au kuifanyia kazi amri ya utendaji nambari 1 iliyotolewa mnamo Mei 22, 2024  na mshatakiwa wa kwanza, wa pili na wa tatu, litakalodumu hadi Julai 8, 2024 wakati ombi hilo litakaposikilizwa na kuamuliwa. Ombi hilo litawsilishwa kwa washtakiwa ndani ya siku 7 kutoka leo,” aliamua Jaji Nguguna.

Kwingineko siku ya Jumatatu Mahakama kuu ya Mombasa iliidhinisha na kutaja kesi sawia na hiyo kupitia jaji Olga Sewe kuwa ya dharura na kuagiza ombi hilo liwasilishwe kwa washtakiwa na majibu ndani ya siku 3 kutoka siku ya kuwasilishwa kwa ombi hilo.

Kulingana na uzito wa kesi hiyo, Mahakama ya Embu itasikiliza na kuamua kessi hiyo Julai 8, 2024 huku Mahakama ya Mombasa ikitarajiwa kutoa maelezo zaidi mnamo Mei 31, 2024.

Ikumbukwe kuwa siku ya jumatatu Mei 27, 2024 rais William Ruto alikutana na viongozi kutoka kaunti ya Embu katika ikulu ya Nairobi kujadili hatama ya marufuku hiyo ya muguka kutoka kwa kaunti tatu za ukanda wa pwani.

Agizo hilo lilipokelewa kwa tabasamu ikiwa ni afueni kwa wakulima, wafanyabiashara na watumiaji wa Muguka.

BY MAHMOOD MWANDUKA