HabariNews

Mfumo wa ugavi wa mapato wa One-man-one-vote-one-shiling wazidi kukashifiwa

Viongozi wa chama cha ANC eneo la kaskazini mwa bonde la ufa wamejitokeza kumsuta naibu wa rais Rigathi Gachagua kufuatia kauli yake ya kuhusu ugavi fedha za kitaifa.

Naibu wa rais Rigathi Gachagua alisema siku kadhaa zilizopita kwamba anaunga mkono kugawanywa kwa fedha za kitaifa katika ngazi ya kaunti kwa kuzingatia wingi wa watu.

Kulingana na Katibu wa chama cha ANC kaunti ya Uasin Gishu Nicholas Adagala ni kwamba iwapo hatua hiyo itashinikizwa na kutekelezwa maeneo mengine yataathirika zaidi hususan yale ameneo yenye rasilimali nyingi.

“Matamshi ambaye imesemwa ya shilingi moja, one man one shilling one vote kuna baadhi ya watu wataathirika kutokana na matamshi kama hayo.

Wakati unasema eti pesa igawanywe kutokana na wingi watu,kuna sehemu hapa Kenya watu ni wachache lakini kuna resources nyingi zinatoka huko,”alisema Adagala.

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu aliungana na viongozi wengine hasa kutoka maeneo Kame ambaye alidai kwamba msukumo huo unatoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kutoka eneo pana la Mlima Kenyahatua ambayo alisema ni hujuma kwa baadhi ya jamii hapa nchini.

Kufuatia mjadala huo, mamlaka ya ugavi wa mapato CRA Mnamo Mei 22, 2024 ilitoa maelezo zaidi.

Kulingana na CRA ugavi wa mapato kutokana na idadi ya watu kama ilivyonukuliwa kutoka kwa naibu wa rais haiwezi kutekelezwa na kwamba mchakato huo unalenga kufanikisha maendeleo kwa usawa kwenye maeneo mbalimbali nchini.

“Kutoka kwa mtazamo wa kitaalamu, pendekezo la mtu-mmoja- kura-moja -shilingi-moja ni kigezo tu lakini hauwezi kuitumia kugawanya mapato. Hatutazingatia pendekezo hilo kwa sababu haikutoka kwa kaunti yoyote.” Alieleza Kamishna wa tume hiyo Hadija Juma.

Kulingana na kuna haja kwa taifa kukumbatia mfumo huo wa one-man-one vote-one-shilling kwani kuna maeneo yenye watu wengi yanapata mgao sawia na mengine ambayo yana idadi ndogo ya wananchi.

BY EDITORIAL DESK