HabariNews

Rais William Ruto Aongoza Maombi Ya 21 Ya Kitaifa Jijini Nairobi

RAIS WILLIAM RUTO AONGOZA MAOMBI YA  21 YA KITAIFA JIJINI NAIROBI.

Rais William Ruto analiongoza taifa katika maombi ya kitaifa yanayoendelea kwenye bustani ya Hoteli ya Safari jijini Nairobi katika hoteli.

Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua waliwasili katika hafla hiyo wakiwa wameandamana na wake zao, Mama wa taifa Bi Rachael Ruto na Bi Dorcas Rigathi mtawalia.

Viongozi wengine Mashuhuri waliohudhuria maombi hayo ni Pmaoja na Mkuu wa Mawaziri Wycliff Musalia Mudavadi, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula na Mwenzake wa Seneti Amason Kingi, wabunge, viongozi wa kidini pamoja na viongozi wengine kutoka mataifa ya nje.

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula alitangaza tarehe ya siku hiyo  ya maombi takriban mwezi mmoja uliopita huku kauli mbiu ya maombi hayo mwaka huu ikiwa ni ‘Matumaini’.

Kulingana na Wetangula, maombi hayo kitaifa huandaliwa na wabunge na inajumuisha viongozi kutoka maeneo mbalimbali nchini nan je ya nchi.

Maombi hayo yamehusisha madhehebu na dini mbalimbali na viongozi kama desturi hutumia furas katika jukwaa la hafla hiyo kuzungumza masuala mbalimbaliyenye amani ya kitaifa, na uwiano wa viongozi katika njanja za kisiasa na dini tofauti.

Wakati huu ambapo wakenya wengi wameendelea kuumia na kulalamikia matozo ya ushuru rais Wiliam Ruto anatarajiwa kuzungumzia kuhusua suala hilo hasa wakati huu ambapo sheria ya fedha yam waka 2024 imeanza kujadiliwa kupitia uhusishwaji wa wanachi katika maeneo mbalimbali nchini.

Desturi hiyo ya maombi ina chimbuko lake takriban miaka 78 iliyopita duniani wakati wa vita vya dunia vya pili wakati ambapo kundi la wabunge wa marekani waliamua kukusanyika kufanya maombi wakati wa vita hivyo dunia.

Maombi hayo ya kitaifa ni ya 21 tangu yazinduliwa hapa nchini mnamo mwaka wa 1986.

BY MAHMOOD MWANDUKA