Wakizidi kuikosoa kauli ya naibu wa rais Rigathi Gachagua ya ugavi wa fedha za kitaifa kuzingatia idadi ya watu katika maeneo mbalimbali nchini, wawakilishi wa wadi kaunti ya Taita Taveta walipinga vikali kauli hiyo na badala yake kupendekeza ugavi huo kuzingatia rasilimali zinazopatikana na ukubwa wa kieneo.
Wakiongozwa na Peter Shambi walisisitiza kwamba endapo mfumo huo utazingatiwa itakuwa na athari kwa maeneo yenye idadi ndogo ya wananchi.
Kulingana nao ya ugavi wa mapato wa One-man-one-vote-one-shilling kama alivyoupigia debe Gachagua, kaunti nyingi zitasalia nyuma zaid kimaendeleo.
“Basi tunataka mfumo ubadilishwa, itoke kwa hiyo yake anasema na sisi tupewe ya One-man-one-shilling-one-kilometer, ili tuweze kuaptiwa mbuga yetu ya wanyama ya Tsavo.
Iweze kurudishwa kwa serikali ya kaunti, sisi wenyewe tumilikituamue ni nani ambaye taenda kuchimba madini huk, tuamue ni watalii watakaoingia mahali pale na tujue kama ni nani yule anacollect yale mambo ambayo yanaitwa Carbon Credit,” alisema Shambi.
Miongoni mwa kaunti zenye idadi ndogo watu hapa nchini ni Pamoja kaunti ya Lamu na Taita taveta katika ukanda huu pwani na kaunti za ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa nchi.
You can also read;http://sautiyapwanifm.com/2024/05/29/mfumo-wa-ugavi-wa-mapato-wa-one-man-one-vote-one-shiling-wazidi-kukashifiwa/
BY EDITORIAL DESK
[…] https://sautiyapwanifm.com/2024/05/29/serikali-imetakiwa-kuzingatia-ugavi-wa-mapato-ya-kitaifa-kwa-u… […]