Naibu wa rais Rigadhi Gachagua amesema kwamba uatawala wa Kenya Kwanza umekuwa utawala wa kwanza nchini kukumbatia maombi kwa manufaa ya taifa.
Akizungumza katika hafla ya maombi ya kitaifa Mei 30, 2024 naibu wa rais alisema kwamba Kenya ilikuwa imekumbwa na kiangazi cha muda mrefu kwa takriban miaka 40.
Kulingana naye utawala wa Kenya Kwanza umekuwa wa baraka kwani kupitia kwa maombi ya kila mara tangu uchaguzi mkuu kufanyika 2022, Kenya imekuwa ikishuhudia neema chungu nzima ikiwemo kupatikana kwa mvua nchini. Aliongeza kwamba kupitia maombi, Kenya ina chakula cha kutosha na taifa linaelekea katika mwelekeo unaofaa.
“Rais William ruto na Mimi, tuliombewa na wakenya wakati wa kuingia kwenye Madaraka na utawala wetu unaendelea kuimarika kutokana na maombi.
Tuliposhika hatamu za uongozi wa taifa tulikuwa na kiangazi kibaya zaidi ndani ya mika 40 baada ya misimu minne mtawalia kufeli, na kupitia maombi Mungu alitueletea Mvua. Kupitia maombi sasa tuna usalama wa chakula na taifa linaelekea pazuri,” Alisema Gachagua.
BY MAHMOOD MWANDUKA