HabariNews

Pigo kwa Mbunge wa Magarini, Akipoteza Kiti cha Ubunge

Mahakama ya upeo imefutilia mbali ushindi wa Mbunge wa Magarini Harrison Garama Kombe ikisema uchaguzi wa agosti nane haukuandaliwa Kwa uwazi.

 Kwenye uamuzi huo, majaji watatu waliosikiliza ombi la Kombe wameshikilia kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama ya rufaa ulioharamisha ushindi wa Kombe.

Stanley Kenga Karisa, alielekea mahakamani kupinga ushindi wa Kombe nakulalamika kuwa zoezi la uchaguzi eneo hilo liligubikwa na visa vingi vya udanganyifu.

Kwenye lalama zake, Kenga alisema madebe ya kubebea kura yaliwachwa wazi katika vituo vingi eneo hilo.

Aliitaka mahakama kuufuta ushindi wa Kombe na kulazimisha zoezi hilo kurudiwa ili wakaazi eneo hilo watendewe haki.

Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi nchini Sasa unatoa nafasi Kwa tume huru ya uchaguzi IEBC kuandaa uchaguzi mdogo eneo hilo wakati wowote kuanzia Sasa.

Aidha akizungumza Kwa njia ya simu, Stanley Kenga amefurahia uamuzi huo akiitaka serikali kuharakisha kuundwa Kwa tume ya uchaguzi nchini ili zoezi hilo liweze kuandaliwa Kwa haraka.

 

BY JOSEPH YERI