Awamu ya tano ya ufukuzi wa maiti msituni Shakahola kaunti ya Kilifi imeanza hii leo shughuli iliyofanywa chini ya usimamizi maafisa wa kitengo cha mauaji ya halaiki katika idara ya upelelezi, DCI.
Mnamo Jumatatu Juni 3, miili saba ilifukuliwa kutoka kwa makaburi matatu na kupelekea jumla ya miili iliyofukuliwa msituni Shakahola kufikia 436.
Ufukuzi wa maiti ulioanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita ulisitishwa Kwa muda kutoa mwanya Kwa zoezi la kutoa miili iliyotambuliwa Kwa familia zao.
Duru za kuaminika kutoka Kwa idara hiyo ya upelelezi zinasema awamu hii huenda zaidi ya makaburi 50 yakafukuliwa.
Miili hiyo tayari imesafirishwa na maafisa hao hadi chumba Cha kuhifadhi maiti Cha hospitali kuu mjini Malindi ikisubiri kufanyiwa upasuaji.
Kulingana na idara ya upelelezi baada ya zoezi hilo shuhuli ya upasuaji itaanza rasmi chini ya uongozi wa mpasuaji mkuu wa serikali Johansen Oduor.Zoezi hilo linaendelea siku ya Jumanne.
BY JOSEPH YERI