HabariNews

Viongozi wa Pwani Waungana Kupiga Vita Muguka eneo la Pwani

Viongozi wa Kisiasa eneo la Pwani kwa kauli moja wameafiki kuunga mkono marufuku ya Muguka iliyotolewa na baadhi ya kaunti za Pwani.

Viongozi hao waliojumuisha wabunge na maseneta wameafiki kusimama kidete kuteta maslahi ya wakazi wa ukanda wa Pwani na hata kuweka tofauti zao za kisiasa kando.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Pwani Dan Mwashako ambaye pia ni mbunge wa Wundanyi, viongozi hao sasa wamepuuzilia mbali kikao na waziri wa kilimo Mithika Linturi, wakiapa kuwa kamwe hawatakakutana na waziri huyo Alhamisi hii kama ilivyopendekezwa na rais Ruto.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano wa Jumatatu Juni 3, ni pamoja na Naibu mwenyekiti wa UDA aliyepia mbunge wa bunge la Afrika Mashariki EALA, Hassan Omar Sarai, Naibu Kiongozi wa wengi bungeni Owen Baya, Seneta wa Mombasa Mohammed Faki, Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga, Mwakilishi wa kike kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu miongoni mwa wengine.

BY NEWS DESK