HabariNews

Taharuki yatanda hakimu akipigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa kikao cha mahakama jijini Nairobi.

Wasiwasi ulitanda katika mahakama ya Makadara jijini Nairobi baada ya Hakimu Monica Kimani aliyekuwa akiendesha kikao cha Mahakama kupigwa riasi.

Tukio ambalo lilitokea mnamo Alhamisi ya 8 Juni katika mahakama ya Makadara jijini Nairobi liliripotiwa kufanywa na afisa wa polisi.

Kwa mujibu wa mafisa wa usalama, Hakimu Monica alipigwa risasi na afisa huyo kufuatia hatua ya kufutiliwa mbali kwa dhamana ya mkewe anayekabiliwa na kesi katika Mahakama hiyo.

Hata hivyo Hakimu Monica alipelekwa hospitalini kupokea matibabu huku duru zikiarifu kwamba afisa huyo aliyemfyatulia riasi hakimu huyo ameuliwa.

Tayari maafisa wa upepelezi wa kitengo wamefika katika eneo hilo kuanzisha uchunguzi kubaini kiini cha mkasa huo.

BY MAHMOOD MWANDUKA