HabariNews

Chama Cha Mawakili Kimejiondoa Kwenye Jopo la Kuchunguza Madeni YaTaifa

Chama cha mawakili nchini kimejiondoa kwenye jopo lililoundwa na rais William Ruto kuchunguza na kutathmini madeni ya taifa Kwa muda wa miezi 90 kikidai kuwa majukumu hayo ni ya mkaguzi wa umma wala sio jopo kwa mujibu wa katiba.

usimamizi wa chama hicho kimeandika notisi ya kuarifu umma kwamba hakuna mwanachama wake atakaejihusisha katika jopo hilo kwani uundwaji wake umekiuka sheria.
Haya yalijiri hapo jana ambapo rais Ruto alimteuwa rais Wa LSK Faith Odhiambo kama mwanajopo la kuchunguza na kutathmini madeni ya Taifa.

Kwenye mahojiano na sauti ya pwani FM mwenyekiti wa mashirika yasio ya kiserikali pwani Zedekiah Adika alisema kuwa jopo hilo halitaweza kutoa suluhu yakutosha ikizingatiwa kwamba limeundwa nje sheria.
Ameongeza kuwa licha ya hayo kuna majopo zaidi ya 3 ambayo kufikia sasa ripoti yao hayajatekelezwa.

BY DAVID OTIENO