Wadadisi wa masuala ya uongozi na siasa ukanda wa pwani wameikosoa hatua ya rais William Ruto kumualika kinara wa azimio kufanya mazungumzo baada ya maandamano ya vijana.
Wakiongozwa na Abdusalam Kassim amesema hatua aliyoichukuwa haikufaa akiwalaumu washauri rais Ruto.
Alisema vijana wa Gen-z kama wenyewe walivyojitambulisha hawana kiongozi na hivyo kuhusisha wanasiasa kwenye mageuzi ambayo vijana wanayashinikiza serikalini huenda likaleta utata zaidi katika taifa la Kenya.
‘’Kiongozi wa upinzani wa upande wa ODM does not represent GEN zs, I think ni desperation ya rais. He made a very big mistake kwa sababu people have seen this and they have always seen kwamba this is how Raila sometimes get on his way,” alisema Abdusalam.
Aidha alitaja hatua ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri kama hatua ya kwanza ya kufanikisha matakwa ya Wakenya lakini huenda ikakosa tija endapo rais Ruto hatakuwa makini wakati wa uteuzi wa baraza jipya.
Kulingana naye rais Ruto anafaa kuhakikisha anachagua wataalamu wenye uwezo wa kufanya kazi badala ya kurudisha wanasiasa ambao lengo lao ni kunyakua mali ya uma kupitia kwa kanadarasi na fedha zinazotengewa wizara mbalimbali.
‘’We need people who will not be there to follow orders ,people who will not be there because of the partie’s interest ,people who are there actually to make sure that the finance ile ambayo inatakikana kutumika inatumika vile inafaa.” Alishauri.
Akizunumzia maandamano ambayo vijana wanaendeleza nchini kiongozi huyo aliwapongeza vijana kwa ujasiri wa kusimama kupinga sera mbovu na uongozi mbaya. Aliwahimiza Gen-Zs kuendeleza maandamano yao ya amani bila kuvunja mali ya uma.
“Hao watu wengine ambao wana biashara ndogondogo wanajaribu kumaintain maisha yao na ya wengine, stop spoiling people’s property.
Msiharibu msiharibu kitu ambayo tumejaribu kutengeneza as Kenya, support us. Kenyans do the peaceful demonstrations, show the anger but msiharibu mali ya watu,”Aliongeza.
Hata hivyo kiongozi huyo alipendekeza rais William Ruto kuwahusisha Wakenya hasa Vijana kupitia mwa wawakilishi wa wadi kwa kufanya vikao vya uhusishaji wa uma’ Public Participation” wanakili kwa maandishi na hata kwa sauti mapendekezo yao na kuyawsilisha kwa serikali kuu.
Alisema hii ndio njia bora zaidi kuliko kuwaalika wanasiasa kutatua masuala yanayoibuliwa.
BY MAHMOOD MWANDUKA