Siku kadhaa baada ya raisi William Ruto kuteua awamu ya kwanza ya mawaziri,wakaazi wa Kaunti ya Kwale hususan wavuvi kutoka Shimoni kaunti wamemtaka raisi Ruto kumteua tena Aliyekuwa waziri wa madini na uchumi samawati Salim Mvurya katika Baraza jipya.
Wakiongozwa na Mohammed Ndalu mmoja wa BMU katika eneo Hilo alisitiza kuwa waziri Mvurya ameonyesha ukakamavu wake katika wizara hiyo hivyo kumuomba kumrudisha katika wizara Ile Ile aliyoitumikia ndani ya miaka miwili.
“Saa hii kama bandari tumepata boti tofauti tofauti hii ni Kwa sababu ya juhudi, nguvu na hekma zake za uongozi na ukiangalia Kaunti zengine kuna aquaculture ambayo ni masuala ya uvuvi na kipindi cha nyuma zilikuwa zimelala lakini kutokana na uongozi wake mzuri nina Imani watu wengi walifaidika”, alisema Ndalu.
kauli yake iliyoungwa mkono na Omar mtengo alisema kuwa tangu Mvurya kuchukua madaraka wavuvi na wahudumu wa bahari walifaidika sana katika kuboresha sekta ya uvuvi ikiwemo maboti ya kisasa.
“Niseme tu Kwanza ,nishukuru Sana raisi Kwa kazi anayoifanya Kwa kuja na baraza jipya la mawaziri nafikiri Kwa weledi wake atachagua mawaziri ambao ni weledi katika shughuli ambazo zinafanyika kwa Kenya nzima,ombi letu kama watu wa kwale tukiwemo wavuvi,tunamuomba raisi kumrudisha mheshiwa Mvurya katika wizara aliyohudumu ili aweze kupeleka gurudumu mbele kulingana na vile alivyofanya kazi zake katika wizara hiyo ya madini na uchumi samawati “, asema Mtengo.
Querean Samuel mmoja wa wamama alisema kuwa kurudishwa kwa waziri Mvurya katika Baraza Hilo kutaleta natija kubwa kwa wahudumu wa bahari katika eneo la Pwani na Kenya kwa ujumla.
Asema Querean , “kuwa kwake waziri kulikuwa na mashirika kama KEMSED lakini hapo mwanzoni tulikuwa hatuoni uwajibikaji wao wa kazi lakini waziri mvurya alipoingia katika wizara hiyo tuliona utendakazi wake,huku kwetu pwani tunategemea bahari katika shughuli zetu za uvuvi ambapo umeboreshwa na sisi wachuuzi wa samaki tumeona jinsi ambavyo biashara ya samaki imefunguka na kufungua masoko ambapo Serikali inafaidika”.
Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wa Pwani pia wakimrai Ruto kuhakikisha Wapwani wanajumuishwa katika Baraza Hilo.
By Bintikhamis Kadide