AfyaHabariLifestyleNews

WAKUU WA IDARA YA AFYA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI.

Wakuu wa vitengo mbali mbali vya afya wamehimizwa kushirikiana na wanahabari ili kurahisisha usambazaji wa taarifa zinazohusu afya kwa umma.

Katika kuhakikisha kuwa wanahabari wanatekeleza majukumu yao ya kuburudisha, kuelimisha na kufahamisha, wito umetolewa kwa viongozi wa idara mbali mbali za afya kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili kurahisisha utendakazi wao.

Kulingana na mratibu wa mipango wa muungano wa wanahabari wanawake nchini AMWIK, Lorna Sempele, mradi wa USAWA unalenga kutoa mwafaka huo pamoja na kurahisisha utendakazi baina ya wanahabari na wadau husika.

Ameeleza kuwa viongozi wa idara za afya kukataa kuwa vyenzo vya habari ama kusaidia kuthibitisha taarifa za afya kunawafanya wanahabari kupitia wakati mgumu wakati wa kutayarisha taarifa hizo.

“Kwa ajili ya kutaka mradi wa USAWA wanahabari kuandika taarifa za kiafya viongozi wa idara mbali mbali za idara ya afya kama vile wakurugenzi wa vituo vya afya, maofisa wa mawasilano katika idara za afya ni vizuri iwapo tutajua tunaweza kusaidiana namna gani ndio waweze kufanya kazi yao bila kusumbuliwa bila kutosikilizwa kwa sababu wakati mwengine wanahabari wanapiga simu kwa wakuu hawa kutafuta taarifa muhimu, wanatuma barua pepe kutafuta habari muhimu za kiafya lakini wanakosa usaidizi wanaambiwa huyo mtu hayuko ama wanaambiwa hapana.” alisema Sempele.  

Sempele hata hivyo amesema wananchi wanawategemea wanahabari kupata taarifa za afya hivyo basi amewataka wanahabari kuhakikisha kuwa wanathibitisha taarifa zao kabla ya kuzipeperusha hewani ili kuepuka kushutumiwa kwa usambazaji wa taarifa ghushi.

Hata hivyo amesema kupitia mradi wa USAWA wanaendelea kutoa mafunzo kwa wanahabari yatakayowasaidia kuwa na ufahamu wakutosha wa maswala ya afya na kutekeleza majukumu yao kwa njia ya utaalamu zaidi.

Kuna njia gani ambayo unaweza kuhakikisha ya kwamba ile taarifa ambayo unaandika kuhusu afya ni ya kweli wala sio taarifa ghushi? lazima tutilie maanani “fact checking”

“Halafu mara nyingi kuandika taarifa za afya inahitaji mwanahabari kufanya utafiti wa kutosha na mara nyingi taarifa hizo hizo huwa kwa lugha ya kisayansi inakuwa vigumu yeye kuandika taarifa hiyo bila yeye mwenyewe kuelewa.” alisema Sempele.

 

ERICKSON KADZEHA.

Comments (1)

Comments are closed.