Katibu mkuu wa chama cha Odm Edwin sifuna sasa amejitokeza na kuwawataka wanachama wane wa chama hicho walioteuliwa kuwa mawaziri katika serikali ya rais William Ruto kujiuzulu.
Akizungumza mnamo 25 July, 2024 kufuatia uteuzi wa baadhi ya wanchama wa chama hicho kushikilia nyadhfa za mawaziri Sifuna alibaini kwamba wanne hao ambao ni Wycliff Ambetsa Oparanya, Hassan Ali Joho, John Mbadi na Opiyo Wandayi waliteuliwa kibinafsi wala sio chama kilichoidhinisha uteuzi huo.
Kulingana na Sifuna ni kwamba kinara wa chama hicho Raila Odinga hakuhusishwa kwenye uteuzi huo na iwapo angehusishwa asingethubutu kuteua majina bila kuzingatia usawa wa kijinsia.
Aliongeza kusema kwamba ni dhahiri shairi uamuzi huo haukutoka kwa chama kwani kufikia sasa hakuna taarifa rasmi ya ODM kuzungumzia uteuzi huo.
“What we want to say is this, I expect that by the end of the day or before they go for vetting we will receive their resignations of these people from their positions in the party because the law is that they cannot go into cabinet as parties and members of political parties.
I’m telling you, this is not a decision of Raila Odinga. It is a decitionmade between these members and the president himself,”alieleza Sifuna.
Hata hivyo kauli ya Sifuna imepingwa vikali na Seneta wa Kisumu Tom Odhiambo Ojienda ambaye alichaguliwa kupitia ODM japo anaegemea upande wa serikali, akisema kuwa ni muhali kwa wanachama hao wakuu katika chama kuteuliwa bila idhini ya kinara wao Raila Odinga.
“I think I disagree with Mr. Sifuna the SG that these individuals were appointed in their individual capacities.
There is no way these four appointees would have joined Government without the nod of the leader of the party.” Alisisitiza Ojienda.
Haya yanajiri baada ya rais William Ruto Jumatano 24 Julai, 2024 kutangaza sehemu ya pili ya baraza lake jipya la mawaziri ambapo alimeza baadhi ya viongozi wenye usemi katika chama cha ODM.
Katika uteuzi huo Ruto alimteua John Mbadi kuwa waziri wa hazina ya kitaifa, Wycliff Oparanya kuwa waziri wa biashara ndogo ndogo na vyama vya ushirika, Ali Hassan Joho kuwa waziri wa Madini na Uchumi wa baharini na Opiyo Wandayi kuwa waziri wa Kawi.
BY MAHMOOD MWANDUKA.