HabariNews

Mawaziri bila Wasaidizi (CAS) Hawawezi Kufanikiwa: Mwashetani Adai Jukumu la Uwaziri ni Zito

Aliyekuwa Msaidizi wa Waziri (CAS) katika Wizara ya Afya, Khatib Abdallah Mwashetani, amebaini kwamba mawaziri ni viongozi ambao majukumu wanayoshikilia katika wizara ni mazito yanayohitaji mawaziri wasaidizi.

Katika mahojiano ya kipekee na Sauti ya pwani Fm Mwashetani alisema sababu ya mawaziri kushindwa kuwajibikia majukumu yao kikamilifu ni kutokana na kulemewa na majukumu na ukosefu wa ushirikiano hivyo kuwawia vigumu kutimiza shughuli zinahusu wizara husika.

“Kuwa na assistant ni kuwa amsaidie kwa kazi, kama vile rais ana msaidizi wake ambaye ni Naibu wake, hizi kazi ni nyingi kwa waqziri peke yake kuzunguka taifa zima ni vigumu.

Sababu kwa nini unaona ni vigumu kupima na kubaini utendakazi wa mawaziri kuwa walifanya vyema au la, it’s because there is a dis-connect of communication,” alibaini Mwashetani.

Licha ya Mwashetani kukiri kuwa wa majukumu yanayotekelezwa na wasaidizi wa mawaziri kuwa ni sawa na majukumu ya Waziri, alisema Waziri husika hawezi kuzunguka taifa zima peke yake kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Ndio, Majukumu ya Waziri ni sawa na majukumu yanayofanywa na wasaidizi wao, lakini, kile ninachojaribu kukwambia, lazima kuwe na msaidizi wa Waziri kwa sababu kazi aliyo nayo ama majukumu katika wizara ni mazito na makubwa, they are enormous.

If you tell me one minister is dealing with two departments and is supposed to be roving around everywhere that is next to impossible, haiwezekani ata struggle, halafu mumwambie haku deliver.”  Alisisitiza

Mwashetani ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Lungalunga aliongeza kwamba vijana wa kizazi cha Gen Z Walikuwa na sababu mwafaka ya kuandamana kushinikiza uongozi bora na sasa wanapaswa kutulia kufuatilia mageuzi ya uongozi yaliyofanywa na rais William Ruto.

Hata hivyo kulingana naye vijana wa Gen Z hawana uzoefu wa uongozi na wanapaswa kuacha Rais na viongozi aliowateuwa Serikalini kufanyia kazi mageuzi waliyoyashinikiza.

Huwezi kutaka Gen-z ako na miaka 19 ukamuweke waziri, hiyo si disaster, miaka 19 mtu umpeleke waziri kwa sababu amepiga kelele kwenye street.

They had valid reason to go to the street na sisi tumeashukuru, because hata serikali rais mwenyewe kama si Gen-z haya mambo yote mabadiliko yasingefanyika,”  aliongeza Mwashetani.

Mnamo Juni 18 vijana kutoka maeneo mbalimbali walianza maandamano yao ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024 kwa kile kilichotajwa kama ushuru wa juu kupita kiasi hasa kwa bidhaa muhimu ikwemo nyongeza ya ongezeko la ushuru wa ongezeko la mapato ya asilimia 16 kwa mkate.

Ni kutokana na vugu vugu hilo la maandamano ya vijana hao ambapo rais aslisalimu amri na kukataa kutia sahihi mswada huo na kutangaza kutupiliwa mbali.

BY MJOMBA RASHID