Wachanganuzi wa masuala ya Siasa na Utawala ukanda wa pwani wametoa wito kwa wananchi kufungua akili zao dhidi ya ulaghai uliojikita katika siasa.
Kulingana na Sheikh Shaban Mwalimu ni kwamba mfumo wa siasa unaotawala nchini na mataifa mengine umegubikwa na uongo hali inayowafanya Wakenya kujipata katika mitego ya wanasiasa ambao hutoa ahadi nyingi kwa lengo la kujipatia kura ili wajinufaishe.
Shabn aliwahimiza wananchi kupima ahadi za wanasiasa wakati wa kampeni iwapo zinaafiki uhalisia kabla ya kuchagua viongozi na baadaye kujutia maamuzi yao.
“Leo kwa mfano Kenya hakuna bishara kubwa hivi sasa ambayo watu wanaekeza zaidi kuuliko siasa.
Tumehujumiwa kimawazo, tukafahamu kwamba siasa si kuhudumikia raia bali kwanza ni kushibisha matumbo yetu.
Sasa hili ndio linakuja katika tafsiri ya kampeni za kisiasa kwamba mimi Shaban Mwalimu ili niweze kupata kura lazima nidanganye.” Alisema Shaban.
Mtaalamu huyo wa utawala hata hivyo aliukosoa mfumo wa uongozi wa kipindi maalumu cha kuhudumu kwa mujibu wa katiba ya Kenya akiutaja kama sababu ya viongozi kujihusisha na ufisadi na kujitajirisha.
Kulingana naye kipindi cha miaka mitano, kiongozi hutumia kujilimbikizia mali akihofia kutochaguliwa tena pindi kipindi chake kitakapokamilika.
Alieleza haja ya kukumbatiwa kwa uongozi unaompa kiongozi muda mrefu wa kuhudumu hadi pale atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake.
“ Kwa sababu miaka mitano ni michache kwa hiyo nitajaribu kupora kwa ile miaka mitano ili pengine miaka mitano mingine ni pata potea.
Kwa hivyo utakuta wanasiasa wakipewa nafasi ndogo, atabidi afanye atakavyofanya hata si mtu mwingine kabisa, yaani yule ambaye uliyemtarajia,” aliongeza.
Kulingana na mfumo wa uongozi katika katiba ya Kenya rais, wabunge, magavana, maseneta miongoni mwa nyadhfa nyingine wanachaguliwa katika uchaguzi mkuu na kuhudumu kwa miaka mitano kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mwingine mkuu kwa wanchi kuchagua viongozi wengine.
BY MAHMOOD MWANDUKA