Wakili Joel Khalende ambaye alitangazwa na kundi linalodai kuwa waasisi wa UDA kuwa katibu mkuu wa chama hicho amejeruhiwa katika makabiliano makali kati ya wafuasi wa kundi hilo na wale wa kaimu katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala.
Kundi hilo lilimtangaza Wakili Khaende kuwa katibu wa chama hicho tawala mnamo 30 Julai, 2024 kuwa katibu rasmi kwa madai ya kupingana na serikali na chama hicho tawala.
Malala mnamo jumanne ya tukio la kutangazawa kubanduliwa kutoka kwenye wadhfa huo alilazimika kujitokeza na kutetea madai kwamba amejiuzulu kama katibu wa chama kupitia kwa barua iliyoonekana ikisambaa katika mitandao ya kijamii akidaiwa kuandikwa barua hiyo.
Kulingana na matukio hayo ambapo Mapema Jumatano ya 31 Julai, 2024 alifika katika makao makuu ya UDA Jijini Nairobi kabla ya makabiliano kati ya wafuasi wake na wale wa kundi linalodai kuasis chama hicho kukabiliana.
Katika tukio hilo maafisa wa polisi walilazimika kuingilia kati kutuliza mvutano huo uliobadilika na kuwa ulingo wa vita kati ya wafuasi wa pande husika.
Hata hivyo Khaende amepelekwa hospitalini kupata matibabu zaidi baada ya kupata majeraha hasa kwenye kichwa chake.
Kulingana na tarifa ni kwamba Malala alifika katika makao hayo makuu ya chama kutaka maelezo ya kubanduliwa kutoka kwa wadhfa huo akishikilia kwamba yeye ndio katibu mkuu wa kitaifa wa UDA hapa nchini.
BY MAHMOOD MWANDUKA