Shirika la Haki Yetu kutoka Kaunti ya Mombasa limekashifu vikali hatua ya serikali kulitishia ili kuondoa kesi dhidi ya waziri wa michezo alipokuwa akihudumu kama waziri wa barabara Kipchumba Murkomen baada ya kuchapisha ushuru wa barabara katika gazeti la serikali kinyume cha sheria. Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Haki Yetu lilishtaki Murkomen Kwa kosa la kutohusisha umma kikamilifu wakati wa kupitisha sheria hiyo.
Kesi hiyo ambayo iliwasilishwa katika mahakama ya Malindi tarehe 31/7/2024 inasema kuwa muda uliochukuliwa kwa zoezi la uhusishwaji wa maoni ulikuwa chache mno na kukiuka katiba. Haki Yetu linasema kuwa majaribio ya serikali kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali yatatikisa utendakazi wao kwani wanafanya kwa wajibu wa sheria na ni sharti katiba iheshimiwe.
Shirika hilo kadhalika limeonyesha kughadhabishwa na hatua ya kesi hiyo kuondolewa mahakamani pasi na kufuata utaratibu wa kisheria
kwa mujibubwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Peter Kiama ,Haki Yetu litasimama kidete hadi pale umma utakapopata haki.
BY DAVID OTIENO