HabariLifestyleNews

Siku ya Vijana Duniani 2024; Magavana Wahimizwa Kuunga Mkono Biashara za Vijana

Huku Kenya ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana, Magavana nchini wametakiwa kuzipa biashara za vijana mazingira bora ka kazi.

Kupitia baraza lao, Magavana wanahimizwa kutozitoza ushuru kwa kipindi cha miezi mitatu biashara za vijana ili kuwapa muda wa kujiimarisha zaidi.

Seneta Maalum kaunti ya Mombasa Miraj Abdillah amemwomba Mwenyekiti wa Baraza la Magavana (CoG) Ann Waiguru kukubali ombi hilo, akisema ni kutokana biashara nyingi za vijana kushindwa kuendelea muda mfupi baada ya kuzianzisha licha ya kupewa mtaji wa kutosha.

“Tusiwe tunawaanzishia biashara halafu zinakuwa frustrated na ushuru baada ya ushuru kuishia kuanguka, sisi tukishawapa pesa za mtaji nyingi zinaanguka bila kupata faida yake.” Alisema.

Akiongea mnamo Jumatatu Agosti 12 katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana katika kituo cha Swahilipot mjini Mombasa, Miraj alisema biashara nyingi za vijana zimeshindwa kuendelea kutokana na ushuru unaotozwa haswa katika hatua za mwanzoni.

Namuomba mwenyekiti wa baraza la magavana awafikirie vijana wa Kenya, sisi tukiwapa mtaji magavana nao wawape muda wa miezi mitatu vijana wetu wanaoanza biashara zao, wasitozwe ushuru kwa muda usio zaidi ya miezi hii (3) wapewe grace period kote nchini.” Alisema.

Miraj aidha alisema tayari amewasilisha mswada katika bunge la seneti ambao utawezeshwa kutunga sheria ya kuwa na Warsha Maalum za umaarufu ‘hall of fame’ ambazo zitakuwa zikitumika kuadhimisha na kutambua mafanikio na michango ya vijana, kina mama na walemavu kupitia kazi zao kwenye jamii.

Nimepeleka mswada wa kuomba kutungwe sheria ya warsha ama kumbi ambazo zitakuwa zikitambua na kusherehekea juhudi za akina mama, vijana na walemavu wanaofanya kazi tofauti tofauti katika gatuzi zetu, the bill inaitwa ‘The county hall of fame’ kupitia mswada huu tutapata vijana wa nyanja zote wa talanta mbalimbali. Vijana wana talanta na tunataka ziangaziwe zote na si soka pekee kama inavyopewa kipaombele kabumbu basin a hizi talanta ngingine ziweze kuangaliwa.” Alisema

Vilevile Miraj amewasihi magavana wa kaunti za Pwani kuzingatia sana rasilimali zilizoko eneo hili ikiwemo bahari kuwawezesha vijana kwa mafunzo mwafaka katika ili iwe rahisi kwao kunufaika zaidi na nafasi za ajira.

Siku ya Kimataifa ya Vijana huadhimishwa kote Ulimwenguni kila tarehe 12 mwezi Agosti; kauli mbiu ya maadhimisho yam waka huu ikiwa ni:Njia za Kidijitali za Vijana kwa Maendeleo Endelevu.’

Maadhimisho ya mwaka huu yakijiri katika chini ya miezi miwili ambapo kumeshuhudiwa wimbi la maandamano ya vijana wa Gen Z waliokuwa wakishinikiza mageuzi, upatikanaji wa ajira na uongozi bora.

By Mjomba Rashid