HabariLifestyleMombasaNews

Wakenya Kulipia Ada za Kutumia Barabara ya Dongo Kundu na Nyinginezo iwapo Sera ya KeNHA Itaidhinishwa

Wakenya sasa wataanza kulipia ada za kutumia baadhi ya barabara kuu nchini iwapo sera ya Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu nchini (KeNHA) itaidhinishwa.

KeNHA, inasema Sera hiyo ya Utozaji Ada za Barabara ambayo kwa sasa ipo katika hatua za majadiliano, itatoa mwongozo kamili wa barabara ambazo zitatozwa ada.

Kulingana na KeNHA, barabara ambazo zitakazowasilishwa kwa ajili ya kuzingatiwa katika sera hiyo ya utozaji ni pamoja na Barabara Kuu ya Thika Superhighway, Nairobi Southern Bypass, Barabara kuu ya Nairobi-Nakuru-Mau Summit, barabara kuu ya Mombasa Southern Bypass na barabara Kuu iliyofunguliwa majuzi mjini Mombasa ya Dongo Kundu Bypass.

Kwa sasa barabara inayolipishwa ada hapa nchini ni ile ya Nairobi Expressway ambayo inasmamiwa na Kampuni ya Moja Expressway ambapo watumizi wa barabara hiyo ya Kilometa 27 hulipa kati ya shilingi 120 na 360 kutumia babarabara hiyo inayopunganisha Uwanja wa ndege JKIA na Nairobi Westlands.

Katika taarifa yake Mamlaka hiyo hata hivyo imewahakikishia Wakenya kuwa Sera hiyo itaundwa kwa kuhusisha kikamilifu wananchi kwenye vikao vya kuchukua maoni ya umma ili kuhakikisha maoni yao yanajumuishwa na kusikilizwa.

Tayari kuna mipango ya kujenga barabara kuu ya njia sita ya Nairobi-Mombasa Expressway itakayopunguza msongamano na kupunguza muda wa kusafiri baina ya miji hii miwili hadi Kenya masaa 4 na nusu na huku Serikali ikiwa imetangaza mipango ya kutoza ada barabara hiyo.

Ikumbukwe kuwa wakati wa ziara ya ya Kiserikali nchini Marekani Rais William Ruto alitia saini mkataba wa shilingi bilioni 463 kujenga barabara kuu yhiyo ya Kilometa 440 ya Mombasa-Nairobi.

By Mjomba Rashid