HabariNews

Wafanyakazi wa nyumbani wapata utetezi

Shirika la kijamii la Youth Alive Kenya limeanzisha harakati za kuhamasisha jamii kuhusu mpango kutambua mchango wa wafanyakazi wa nyumbani hususan maswala ya malipo.

Shirika hilo linatekeleza mpango huo uitwao Time to care project katika kaunti za MombasaNairobiKiambu na Nakuru unaofadhiliwa na serikali ya Canada kupitia shirika la Oxfam Kenya.

Afisa wa mipango katika shirika hilo Rahma Issa, alisema serikali za Kaunti zinajukumu kubwa kuhakikisha zinatekeleza sera za kulinda wafanyakazi wa Nyumbani.

Rahma Vile vile alishinikiza serikali kuu kuharakisha utekelezwaji wa sheria za kuangazia hamasa kuhusu kuinua wanawake kiuchumi.

“Youth alive Kenya by the funding from governmrnt from Canada through Oxfam Kenya we are implementing time to care project ambayo malengo yao makuu ni kuhakikisha the burden of unpaid care work imeweza kupungua na serikali zetu zimeweza kuekeza fedha ili kuhakikishan maswala ya care infrastructure imewez kuwa in place. Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo vinatuweka nyuma nah ii ni maswala kama kuratify the convection C189 ambayo inaprotect the right of domestic workers, so ingekuwa bora kama nchi tuweze kuspeed up hii ratification ya convection C189 ambayo inatetea haki ya wafanyakazi”, alisema Rahma.

Rahma Issa, Afisa wa Mipango katika shirika la kijamii la Youth Alive Kenya

Afisa huyo alisema idadi kubwa ya wanawake nchini wanafanya kazi zisizo na malipo na ambazo haichangii maendeleo na uchumi wa Taifa swala ambalo serikali inafaa kuliangazia.

“Napia kuna care policies ambayo serikali yetu imetekeleza kupaumbele, lengo letu ni kuhimiza serikali kuimpliment hizi policies ambazo tuko nayo zenye zinahusiana na maswala ya care ikiwemo pia pia women economic empowerment policy, utapata wanawake wanatumia mda mwingi sana kufanya kazi ambazo hazina malipo, that is unpaid care job, huu mda wangeweza kutumia kufanya maswala yenye yanafaida,yenye yanafaidi nchi yetu kama Kenya, iwapo mimi kama mwanamke nitaamka asubuhi nioshe vyombo nipanguse nifanye kazi zote zile za nyumbani na sijihusishi na maswala ya governance, utapata wanawake wengi issues zetu hazitawekwa mbele kwa sababu hakuna yule ambaye atakuzungumzia kwa nafasi ambayo haumo, so nivizuri kama serikali iweze kuwajibika na kuweka haya maswala mbele”, aliongeza Rahma.

Mwelekezi katika shirika la Kijamii la Manyunyu eneo bunge La Kisauni kaunti ya Mombasa-Ali Sudi Boti, alisema jamii hasa waajiri wanafaa kubadili mwelekeo wa kugawa majukumu kwa wafanyakazi ili kuwe na usawa katika maswala ya maendeleo.

Mwanamke anaweza kufanyakazi zaidi ya masaa matano kwa siku na nikazi ambazo sizakulipwa-unpaid care work, halafu ukiangalia sisi wanaume wengi tunatumia kama saa moja ama labda chini ya saa moja katika kufanya kazi ambazo ni za nyumbani, sasa hii ni kumaanisha kwamba tumemlemeza mwanamke wakati hata yeye pia ni binadamu kama sisi, na nikazi ambazo hata zengine tunaweza kusaidiana, ndiposa tunajaribu kuelimisha wanajamii hususan wafanyakazi na wale waajirim wao kwamba nimuhimu katika kugawanya hizi kazi, ni muhimu kwanza katika nyumba watu wajaribu kurespect na kurecognize hizi kazi ambazo mwanamke anafanya”, alisema Boti.

Wakati huo huo afisa wa chama cha kutetea haki za wafanyakazi Kudheiha Munira Mohammed, anasema wafanyakazi wengi wa nyumbani wamekosa kufahamu haki zao hususan mishahara huku waajiri wakizidi kuwakandamiza.

Alipendekeza wafanyakazi kujisajili katika muungano ili kupata utetezi wanapopitia visa vya dhulma.

Mfanyakazi wa nyumbani anatakikana yule tajiri wake amuangalie ule mshahara ule wa serikali saa hii ambao ni shilingi e17,500, lakini utakuta matajiri wengi mfanyakazi wake atampatia shilingi elfu 6,500, anayelala pale mshahara wake huwa ni shilingi 15,000, huwa wanafaa kuja kwa ofisi zetu wanakuja kuturipotia halafu tunachukua jukumu sasa la kumpatia ujumbe tajiri halafu tajiri anakuja kwa ofisi zetu halafu tajiri anakuja tunaungana, mfanyakazi wake nay eye mwenyewe tunasuluhisha ile kesi”, alisema Munira.

Afisa wa Mipango katika Shirika Hilo la Youth Alive Kenya Rahma Issa anasema utafiti unaonyesha wanawake wa mashinani wanateseka zaidi haswa wanapopata ajira za vijakazi majumbani.

Geophrey Kithuku ni mwakilishi katika Shirika la The Amplifiers Youth hapa Mombasa.

Ni sawa kuwaleta the employers na the employees on care work ili kuweza kuhamasishwa maswala ya bajeti ili wakaweze zile issues around unpaid care work, domestic work zikaweze kuangaziwa katika policies including the budget kwa sababu kwa mda mrefu maswala ya care work yamekuwa yakipewa kisogo, na ukiangalia kuna so many issues ambazo zinatokea pale lakini haziangaziwi”, alisema Kithuku.

BY JOSEPH JIRA