Mashirika yasiyo ya kiserikali ukanda wa pwani yamepinga vikali mapendekezo katika mswada wa ugavi wa rasilimali za kaunti 2024 ya kutaka kupunguza mgao wa fedha kutoka bilioni zaidi ya 410 hadi bilioni 380 yakidai kuwa mapendekezo hayo yatahukumu utendakazi za serikali za kaunti.
kwenye mazungumzo na vyombo vya habari hapa mombasa mombasa mashirika hayo yamesema kuwa uamuzi huo utaathiri utendakazi wa serikali za kaunti ikizingatiwa kuwa hadi kufikia sasa serikali hizo hazijapata fedha huku wakiitaka serikali kutumia mapendekezo ya mamlaka ya kusimamia ugavi wa rasimali nchini cra.
mwenyekiti wa shirika hilo Zedikiah Adika amelitaka bunge la seneti kufwatilia mapendekezo kwamba majukumu ya serikali za ugavi kugatuliwa kikamilifu kama alivyoahidi rais wiliam ruto.
adika kadhalika amezitaka serikali za ugatuzi kufanikisha ufanisi wa ugatuzi kwa kutumia fedha kwa njia inayofaa.