Rais William Ruto na aliyekuwa mpinzani wake wa kisiasa Raila Odinga hatimaye wamewasili jijini Beijing nchini China tayari kuhudhuria Kongamano la Ushirikiano wa China na Afrika.
Katika picha zilizosambaa mtandaoni na kuashiria umoja wao, zimeonesha wawili hao wakishuka jioni hii katika ndege ya Kenya Airways wakiongozana na kulakiwa ujumbe wa China.
Viongozi hao wawili ambao usuhuba wao wa hivi punde umeonekana kushamiri katika miezi ya hivi karibunni ni sehemu ya wajumbe wakuu na muhimu wa viongozi wa Afrika wanaohudhuria Kongamano hilo.
Kufika kwao kwa pamoja kumevutia hisia hasa baada ya mwonekano tofauti wa kifasheni wa rais Ruto aliyeshuka akiwa amevalia shati la kawaida la mikono mirefu aina ya Tommy Hilfiger sweatshirt na suruale ndefu aina ya jeans pamoja na viatu vyeupe maarufu sneakers.
Uwepo wa Odinga katika mkutano huo wa viongozi wa hadhi ya juu unaashiria mabadiliko muhimu katika siasa za Kenya baada ya miaka mingi Raila akiwa mpinzani mkuu wa Ruto kwa kukataa matokeo ya uchaguzi .
Hata hivyo katika kongamnao hilo rais Ruto anatarajiwa kutia saini mikataba ya mamilioni ya dola itakayofanikisha maenddeleo katika miundomsingi na biashara, huku Raila akitarajiwa kukutana na viongozi wa Afrika kusaka uungwaji mono katika azma yake ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.
BY MJOMBA RASHID