HabariNews

Rais Ruto Aelekea Ziara ya siku 2 nchini Ujerumani

Rais William Ruto ataondoka nchini Alhamisi jioni kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini Ujerumani.

Ziara hii inatajwa kuashiria hatua muhimu katika uhusiano wa muda mrefu kati ya Kenya na Ujerumani uliodumu kwa zaidi ya miaka 60 na inalenga kuimarisha uhusiano wa kitamaduni, kiuchumi na kidiplomasia.

Kulingana na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed, Rais Ruto akiwa Ujerumani atajihusisha na shughuli kuu zinazotarajiwa manufaa ya haraka kwa Wakenya.

Rais atashuhudia utiaji saini kwa Mkataba wa Kenya na Ujerumani kuhusu ‘Ushirikiano Kamili wa Uhamiaji, mkataba ambao unatajwa ndio utakuwa kivutio kikuu cha ziara hiyo nchini Ujerumani, mkataba utakaotoa nafasi ya wakenya kupata ajira nchini humo, na mafunzo ya wanafunzi na masuala ya wafanyakazi.

Aidha katika ziara hiyo ya siku mbili rais pia atahudhuria na kuhutubia tamasha la Kila mwaka la “Bürgerfest” lililo na kauli mbiu “Pamoja – Stronger Together,” huku Kenya ikiwa nchi mshirika rasmi, na nchi ya kwanza isiyo ya Ulaya kuchaguliwa kwa jukumu hilo.

Rais Ruto aidha anatafanya vikao vya mazungumzo baina ya mataifa haya mawili ambapo atajadiliana na rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier [SE1] na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuhusu kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kawi ya kijani na hali ya anga, biashara na uwekezaji, leba na masuala ya amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

By Mjomba Rashid