Raia mmoja wa Marekani amefikishwa katika mahakama ya Malindi mapema Jumatatu na kushtakiwa na makosa kuwanajisi watoto katika Kijiji Cha Gede kaunti ndogo ya Malindi.
Mahakama imeelezwa kuwa Antoine Alexander Ziegler amekuwa akiwafanyia unyama huo watoto wa umri wa kati ya miaka 10 na 14 wanaoishi katika nyumba yake.
Inadaiuwa kuwa kwa kipindi cha miaka mitano mshukiwa huyo amekuwa akiwadhulumu watoto hao Kwa kuwatishia kuwatoa katika msaada anaodaiwa kuwapa wao pamoja na wazazi wao.
Mbele ya hakimu Joy Wesongo, Ziegler alikana makosa yote 11 ya unajisi huku mahakama ikikataa kumwachilia Kwa dhamana.
Hata hivyo ombi lake la kuachiliwa Kwa dhamana limepingwa vikali na upande wa mashtaka ukuongozwa na Joseph Mwangi aliyedai huenda mshtakiwa akatoroka endapo ataachiliwa.
Kesi hiyo imeratibiwa kutajwa tarehe 27 mwezi huu.
Haya yanajiri huku msako ukiendelezwa kumsaka mshukiwa mkuu wa unajisi, Michael Balentine raia wa Afrika Kusini, aliyetoroka nchini baada ya kudaiwa kuwanajisi watoto.
Kenya inashirikiana na Polisi wa Interpol kumsaka jamaa huyo huku kibali cha kukamatwa kwake kikitolewa kwa nchi wanachama 176.
By Joseph Yeri