HabariLifestyleNews

Washukiwa Wanne Katika Kesi ya Ulawiti wa Mwanablogu Mombasa Kusalia Korokoroni hadi Alhamisi

Washukiwa wanne wa ulawiti wamefikishwa mahakamani Shanzu mjini Mombasa kujibu mashtaka ya utekeji nyara na ulawiti wa mwanablogu mmoja.

Washukiwa hao wakiwemo wanawake wawili na wanaume wawili wanadaiwa kushiriki utekeji nyara na kulawitiwa kwa mwanablogu maarufu Bruce.

Washukiwa hao Abdul Hassan Sindimba, Haji Babu Mohamed maarufu Achkobe, Esther Muthoni maarufu Tatuu  na Violet Adera (Vayo) hata hivyo wamekanusha mashtaka yanayowakabili.

Mahakama imeagiza wasalie korokoroni hadi Alhamisi Septemba 26, ambapo hatma kuhusu dhamana yao itakapobainika, baada ya upande wa mashtaka kupinga kuachiliwa kwa dhamana.

Upande wa mashtaka umesema mikakati ya kuwasaka na kuwafikisha kortini washukiwa wengine 15 inaendelea.

Irene Karuga Afisa wa Polisi aayeshughulikia kesi hiyo amesema idara hiyo itahoji na kuchukua maelezo ya wanasiasa maarufu akiwemo Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, mama yake mzazi na maafisa wengine wakuu wa serikali ya kaunti ya Mombasa waliohusishwa na kesi hiyo.

Mheshimiwa Jaji, juhudi zinaendelea kuwakamata washukiwa wengine waliobakia, kuandikisha taarifa ikiwemo ile ya Gavana wa Mombasa, mama yake na maafisa wengine wakuu wa serikali ya kaunti ya Mombasa.” Alisema Afisa huyo.

By Mjomba Rashid