Serikali ya Kenya Kwanza ilipata pigo kwa mara nyingine baada ya mahakama kuu kuitangaza sheria ya ubinafsishaji ya 2023 kuwa kinyume cha sheria.
Mahakama kuu ya Milimani Jijini Nairobi mnamo September 24 iliamua kwamba sheria hiyo ambayo ilitoa nafasi kwa mashirika 11 ya serikali kubinafsishwa ilifanywa kinyume cha kanuni na katiba ya Kenya.
Jaji Chacha Mwita wa Mahakama hiyo aliitaja sheria hiyo kwa ujumla wake kuwa kinyume cha katiba baada ya sheria ya ushirikishwaji wa uma kukiukwa.
“A declaration is hereby issued that the National Assembly did not conduct reasonable, meaningful, adequate and effective public participation before passing the privatization act 2023.
The entire privatization act 2023 is therefore, unconstitutional, null and void” Jaji Chacha Mwita aliamua”.
Licha ya Jumba la mikutano la KICC kuwa na umuhimu mkubwa kwa taifa, serikali ya Kenya Kwanza ililenga kuliuza.
Hata hivyo katika uamuzi wake Jaji Chacha aliliokoa Jumba hilo.
“The decision to privatize Kenyatta International Conference Centre or Kenyatta, a national Monument contravenes article 10 (2) of the constitution, led with provisions of the monument and heritage act and is therefore is unconstitutional, unlawful and void.” Jaji chacha alieleza.
Uamuzi huo unajiri kufuatia kesi ya kupinga iliyowasilishwa na chama cha ODM kupinga mchakato wa kubinafsishwa baadhi ya mashirika ya serikali ikieleza kuwa baadhi ya mashirika hayo hayafai kumilikiwa na watu binafsi kutokana na umuhimu wake na usalama wa kitaifa.
Rais William Ruto takriban mwaka mmoja uliopita alitia saini mswada huo na kuwa sheria baada ya bunge la kitaifa kuupitisha na kuwa sheria.
Ikumbukwe kuwa sheria hiyo iliundwa kurekebisha sheria iliyokuwepo ambapo ni lazima mchakato wa kubinafsishwa kwa shirika la serikali au mali ya uma upitie katika bunge la kitaifa.
Serikali iliona haja ya kuondolewa kwa kikwazo hicho na hivyo kuwasilisha mswada huo ili kuipa nafasi serikali kubinafsisha shirika lolote bila bunge kuhusishwa.
Hata hivyo, licha ya kupitishwa kwa sheria hiyo, sasa mashirika yote 11 yaliyolengwa kubinafsiswa ikiwemo; Jumba la KICC, Kampuni ya Kenya Pipeline, Kampuni ya Kenya Seed, Shirika la Kenya Literature Bureau miongoni mwa mengine sasa yameokolewa, na sasa yatendelea kusimamiwa na serikali baada ya mahakama kuiharamisha sheria hiyo.
BY MAHMOOD MWANDUKA