Naibu Rais Rigathi Gachagua amekimbizwa hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Wakili Mkuu tajika Paul Muite anayemwakilisha Gachagua katika kesi inayomkabili ameliambia bunge la Seneti kuwa mteja wake asingeweza kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa anaumwa na alikuwa amefikishwa hospitalini.
Amelitaka bunge kumpa muda was aa mbili au tatu kufika hospitali kutathmini hali halisi aliyo nayo Naibu wa Rais kisha kurejea bungeni.
Spika Amason Jeffwa Kingi amekubaliana na ombi hilo na kuamua kusitisha kikao cha alasiri kwa muda hadi mwendo wa saa kumi na moja jioni watakapobaini uhalisia kamili.
Kingi hata hivyo amesema kutokana na shughuli hiyo kuwa na wakati finyu na mchakato unaozingatia wakati, bnge la Seneti linatarajia Naibu wa Rais kufika bungeni humo mwendo huo was aa kumi na moja kutoa utetezi na ushahidi wake.
“Baada ya kuzingatia pande zote mbili, maagizo yangu ni kwamba tunasitisha vikao kwa sasa hadi saa kumi na moja jioni. Tunatarajia Naibu rais kufika hapa kutoa utetezi na ushahidi wake kwa kuwa mchakato huu unaofungamana na wakati.” Aliamua Kingi.
By Mjomba Rashid