HabariNews

Serikali Yaahidi Shilingi Bilioni 1.5 Kukabiliana na tatizo la Uskwota Pwani

Huenda Tatizo la uskwota na umiliki wa ardhi Pwani huenda likapata suluhu Serikali itakapofanikisha mpango wa ununuzi wa ardhi zinazomilikiwa na mabwenyenye.

Akizungumza katika sherehe za 61 za Siku kuu ya Mashujaa huko kaunti ya Kwale Rais Ruto amesema tayari shilingi bilioni 1.5 zimetengwa kuanza mpango wa kununua ardhi zinazomilikiwa na watu binafsi.

 “Tumekuwa na donda sugu la mambo ya ardhi. Nataka niwatangazie kwamba tayari tuko na pesa shilingi bilioni moja na nusu kuanza mpango ya absentee landlords na kusaidia wananchi ambao wanaishi katika mashamba ambayo si yao, tuweze kuwasaidia waache kuwa maskwota wawe wenyeji.”

Amesema mchakato huo utaendelezwa kwa ushirikiano na viongozi maeneo husika ambapo Serikali itashirkiana na wamiliki wa mashamba hayo na kuyanunua kuyakabidhi kwa wananchi kupata makao.

Tutaungana na wale ambao mashamba ni yao tuweze kuyanunua tuwagawie wananchi ndio tuweze kusomba mbele pamoja.” Akasema.

By Mjomba Rashid