HabariNews

Mshukiwa Mkuu katika kesi ya Ulawiti wa Mwanablogu Mombasa Akamatwa Lungalunga

Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai mjini Mombasa imethibitisha kumkamata mmoja wa Washukiwa wakuu wa utekaji nyara na ulawiti wa mwanablogu Bruce Khajira maarufu Chawa-001.

Mshukiwa huyo kwa jina Omar Ali Mohammed maarufu kama ‘Nyanya’ amekuwa mafichoni tangu kuripotiwa kuhusika katika kitendo hicho cha Septemba 12.

Mohammed amekamatwa na maafisa wa Upelezi kwa ushirikiano na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji katika mpaka wa Lungalunga kaunti ya Kwale alipokuwa akijaribu kutoroka kuelekea nchi jirani ya Tanzania.

Maafisa wa idara hizo wamekuwa macho na wlaikuwa wamepata fununu za mipango ya washukiwa wa kitendo hicho cha kinyama kutaka kutoroka nchini.

Ripoti kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI imeeleza kuwa Omar ni mmoja wa washukiwa wakuu wa kitendo hicho huku uchunguzi wa kidigitali wa kimaabara ukionyesha, jamaa huyo alikuwa kwenye eneo la tukio na kabla ya tukio pamoja na mawasiliano ya njia ya simu na washukiwa wengine.

Aidha gari aina ya Nissan Note lenye nambari za usajili KDQ 394C linaloaminika kutumika kumbeba mwanablogu huyo kutoka Bamburi hadi sehemu alikotekelezewa unyama huo pia limepatikana na kutambuliwa.

Gari hilo linaaminika kukodishwa na Omar kutoka kwa mmiliki mnamo Agosti 20, 2024 na akalirejesha jioni ya Septemba 12 baada yasiku ya tukio hilo na baadaye akalirejesha.

By Mjomba Rashid