HabariNews

Gavana wa Mombasa Awasuta Viongozi Wanaodai Kaunti Ilirejesha fedha Serikali Kuu

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewakemea vikali baadhi ya viongozi wa kisiasa hapa Mombasa aliowataja kueneza uvumi na propaganda wakidai kuwa kaunti imeshindwa kufanikisha maendeleo.

Gavana Nassir amesema wanasiasa hapa Mombasa wanaeza propaganda kwa kudai kuwa kaunti ya Mombasa imerejesha mgao wa fedha mgao kutoka kwa serikali badala ya kutumika kufanya maendeleo.

Nassir amepuuzilia mbali uvumi huo akiutaja kama uchochezi, akisema serikali ya kaunti ya Mombasa Kwa sasa ina takribani miezi 3 haijapokea mgao wa fedha kutoka kwa serikali kuu.

Nimesikia mitandaoni wengine wakiongea ati fedha za kaunti zilirejeshwa Serikali kuu. Acha niwaambie hao, saa hii tumeingia mwezi wa 3 Serikali Kuu haijatuma pesa kaunti ya Mombasa, waache kusema urongo, utapeli lugha ya kuchochea.”

Aidha amesema licha ya kucheleweshwa kwa mgao fedha kutoka kwa hazina kuu, wafanyakazi wa kaunti wanalipwa kwa wakati ufao kupitia ushuru kaunti wanaokusanya.

Hata kama ni Kenya nzima kaunti hazijapewa fedha, Mombasa tunajigamba leo madaktari wote wanalipwa mshahara kwa wakati, wakandarasi waliojenga barabara wanalipwa haki yao on time, na hizi fedha tunazitoa licha ya pesa hazijatoka serikali kuu.

Wale wenye kuwatuma tunaawambia wawatafutie vijana kazi musiwatume vijana waharibu program ya Mombasa yangu bure.” Akasema Nassir.

By Mjomba Rashid