Naibu Rais Prof. Kithure kindiki ameongoza kikao chake cha kwanza cha Baraza la Mawaziri katika makao yake rasmi ya Karen jijini Nairobi.
Mkutano huo kuhusu uongozi, masuala ya jamii na uawala wa umma unajiri wiki mbili baada ya kuapishwa kuwa Naibu Rais kufuatia kutimuliwa afisini kwa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.
Mkutano huo wa Mawaziri umehudhuriwa na mawaziri John mbadi wa fedha, Julius migosi wa elimu , Waziri wa maji Eric Murithi Muuga na Beatrice Askul wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamona na maendeleo ya Kikanda.
Vilevile Waziri wa Vijana na Michezo Kipchumba Murkomen, Rebbeca Miano wa Utalii na Wanyamapori, Debora Mulongo Baraza wa afya, Dkt. Alfred Mutua wa Leba na mwenzake wa Ulinzi Soipan Tuya.
Wengine waliohudhuria ni Mwanasherika Mkuu wa Serikali Dorcas Oduor pamoja na Katibu wa baraza la Mawaziri Mercy Wanjau.
By News Desk