Mamlaka ya Barabara Kuu nchini (KeNHA) imetangaza kufunga kwa muda sehemu ya Barabara Kuu ya Mombasa-Nairobi kati ya Daraja la Makupa na Changamwe Interchange.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa (KeNHA) Mhandisi Kung’u Ndung’u barabara hiyo itakumbwa na usumbufu wa trafiki na kutatizika kwa shughuli za kawaida katika eneo hilo kuanzia Jumapili Novemba 17 hadi Jumapili ya tarehe 1 Disemba mwaka huu.
KeNHA imesema kuwa hatua ya kufunga barabara hiyo kwa muda ni kuruhusu ujenzi wa barabara na kazi za ukarabati wa mifumo ya Mabomba ya majitaka ili kuhakikisha muunganisho mzuri kati ya daraja hilo la Makupa na eneo la Changamwe.
Wakati uo huo KeNHA imewasihi madereva kufuata mipango ya kudhibiti trafiki iliyopendekezwa katika maeneo hayo pamoja na kushirikiana na maafisa wa trafiki barabarani katika eneo hilo ili kuhakisha kazi inakamilika ndani ya muda unaohitajika.
By Mjomba Rashid