HabariNews

Serikali ya kaunti ya Kilifi yawekeza shilingi milioni 300 kukabiliana na uhaba wa maji Kaloleni

Eneo bunge la Kaloleni ni miongoni mwa maeneo kame zaidi kaunti ya Kilifi, wakazi wakitaabika miaka nenda miaka rudi kwa tatizo la uhaba wa maji. Lakini sasa dalili za kupata suluhu ya kudumu kwa tatizo hilo imeanza kuonekana kufuatia serikali ya kaunti ya Kilifi kuwekeza takriban shilingi milioni 300 kuhakbiliana na uhaba wa maji Kaloleni.

Tangu taifa hili kujinyakulia uhuru wake wakazi wa eneo hili hawajapata afueni ya tatizo hili la uhaba wa maji, wakazi wakilazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta bidhaa hiyo.

Omar Said waziri wa maji, mazingira na usafi kaunti ya Kilifi ameeleza kuwa changamoto ya uhaba wa maji eneo la Kaloleni inatokana na uhaba wa umeme unaoshuhudiwa katika kituo cha kusukuma maji cha Mwavumbo kaunti ya Kwale kinachosambaza maji katika eneo bunge la Kaloleni, kwani ni transfoma moja inayotumika kusukuma maji mpaka Kaloleni na vile vile kusambazwa kwa matumizi ya wakazi wa kaunti ya Kwale ambao idadi yao imeongezeka eneno hilo.

Amesema licha ya mabomba makubwa ya kusambaza maji kutoka Mwavumbo hadi eneo bunge la Kaloleni kuwekwa, milima na mabonde mengi inayopatikana katika eneo bunge hilo hufanya kiwango kikubwa cha umeme kutumika kusukuma maji, jambo ambalo limekuwa changamoto kwani udogo wa transfoma unashindwa kuhudumia wakazi pamoja na kituo hicho cha kusukuma maji.

Uhaba wa nguvu za umeme pale Mwavumbo na kama tujuavyo eneo bunge hili lina milima na mabonde mengi, sasa kwa ile changamoto ya umeme tuliyonayo kule Mwavumbo maji hayawezi kufika huku mpaka yasukumwe. Na tunajua kuwa umeme wa eneo lile unasimamiwa na serikali ya kaunti ya Kwale kwa hivyo ni swala ambalo limetupa changamoto kwa kuwa serikali ya kaunti ya Kwale wanatumia umeme ule, idadi ya wakazi wa Kwale imeongezeka eneo lile na sisi kama KIMAWASCO pia tunatumia umeme ule na mabomba yetu ni makubwa jambo hili imepelekea kushuhudiwa kwa uhaba huo wa umeme.” alisema Omar.

Waziri huyo wa idara ya maji na mazingira ameeleza kuwa mikakati inaendelea kati ya serikali ya kaunti ya Kilifi na kampuni ya kusambaza umeme ya Kenya Power kuona kwamba transfoma maalum inawekwa ili kusaidia kasukuma maji kutoka kaunti ya Kwali hadi Kaloleni mkakati huo ukikisiwa kuwa na gharama ya shilingi milioni tatu.

Aidha amesistiza kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi imewekeza takriban shilingi milioni 300 katika eneo bunge la Kaloleni pekee ili kutatua changamoto hiyo ya uhaba wa maji.

Kwa hivyo tunafuatilia swala hili na kampuni ya kusambaza umeme Kenya Power tuweze kupata transfoma yetu peke yetu kama kaunti ambayo watatuwekea pale Mwavumbo. Nimeongea na mkurugenzi wa mauzo wa kampuni hiyo ya Kenya Power na amenieleza kuwa kwa hilo kufanyika gharama yake ni shilingi milioni 3. Japo tunaendelea na mazungumzo tuone tutasaidiana namna gani hata ikiwa tutafanyiwa kwa mkopo ili watu wetu wapate maji.

“Uwekezaji wa mipango ya maswala ya maji ambayo tumeweka hapa Kaloleni ni zaidi ya shilingi milioni 300 ili tupate suluhu ya kudumu ya tatizo hili la uhaba wa maji.” alisema Omar.

Diwani wa Mwanamwinga Edward Ziro ameeleza kufurahishwa na juhudi zinazofanywa kukabiliana na  changamoto hiyo vile vile akisema shida ya maji inayoshuhudiwa eneo bunge la Kaloleni, inatokana na kukosekana kwa vyenzo vya maji vya kutegemewa.

Pia amebainisha kuwa mfumo wa mabomba ya kusambaza uliotumika umesababisha changamoto hiyo kwani mabomba hayo ni madogo na kuleta ugumu wa kusuma maji kutoka Mwavumbo ama Baricho.

Ile shida ambayo imetukumba hapa kwetu eneo bunge la Kaloleni ni kwamba hatujakuwa na vyenzo vizuri vya kutusambazia maji kama jamii ndio maana tumekuwa tukihangaika sana kutafuta maji hasa katika wadi za Kayafungo na Mwanamwinga. Lakini nikiangalia zile juhud ambazo zinafanyika saa hii huwa nasema ndani yah ii miaka mitano inayokuja kutakuwa na mabadiliko  kwasababu  tunatafuta vile vyenzo viliko ili tutoe maji wenyewe huko.

“Kaunti ya Kilifi tunategemea kupata maji kutoka sehemu mbili, Mzizima na Baricho na tatizo ni kwamba mfumo wetu wa mambomba ya kusambaza maji ni madogo sana na inakuwa shida kusukuma maji.” alisema Ziro.

Erickson Kadzeha