HabariNews

Kenya Yapokea Vifaa Vipya vya Angani Kuimarisha Vita dhidi ya Ugaidi

Taifa la Kenya limepokea Vyombo vya kivita 6 vya angani aina ya Bayraktar TB2 ili kuzidisha uimara wake wa kukabili  ugaidi na uhalifu wa kupangwa.

Mashini hizo ambazo zitatumika kwa uchunguzi zimetengenezwa nchini Uturuki na kampuni ya Uturuki ya Türkiye Baykar.
Vyombo vya habari vya Uturuki vilisema hatua hiyo inaashiria kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi hizo mbili.

Vyombo vipya vya kivita vya angani aina ya Bayraktar TB2

Vyombo hivyo vya anga vya Bayraktar TB2, vimethibitishwa kutumika katika migogoro kama vile Nagorno-Karabakh, Libya,
Syria na Ukraine, na vina droni na kamera kali za Aselsan Aselfl ir-500 EO/IR/LD, zinazoimarisha uwezo wao wa ufuatiliaji matukio
na ulengaji shabaha kwa umahiri.

Wanafunzi wa Kenya walikamilisha mafunzo yao ya kutumia vyombo hivyo na droni katika Kituo cha Mafunzo ya Ndege cha
Baykar huko Keşan mnamo Agosti 23 mwaka jana. Kenya inajiunga na mataifa kadhaa ya ya Afrika, yenye vyombo
hivyo spesheli vya kukabili ugaidi ikiwa ni pamoja na Burkina Faso, Togo, Niger, Nigeria, na Morocco.

Vyombo hivyo vya anga vya TB2 hutumika kupambana na waasi, kulinda mipaka na kuimarisha usalama wa taifa, Kenya ikitarajiwa
kujumuisha vyombo hivyo vya anga katika operesheni zake za kijeshi, haswa dhidi ya wanamgambo wa al Shabaab.

Vifaa hivyo vya droni vimegharimu Kenya takribani shilingi bilioni 4, ambapo kila kifaa kinakadiriwa kuwa shilingi Dola Milioni 5 kwa
kila kimoja.

By Mjomba Rashid