HabariNews

Suitofahamu Yagubika Wazazi; Hatma ya Shule 348 Zilizofungwa Ikisalia Mashakani

Huku Wanafunzi wanapojiandaa kurejelea masomo wiki ijayo, shule za msingi 348 zi katika njia panda na hali ya
siutofahamu baada ya Wizara ya Elimu kuamuru kufungwa kwa sehemu za mabweni.

Shule hizi zilishindwa kufikia viwango muhimu vya usalama na kufuata tathmini za kina zilizofanywa mnamo Septemba na
Oktoba 2024.

Huku wakurugenzi wa shule za kibinafsi na walimu wakuu wakitoa hoja zao, wazazi wameachwa katika hali ya
kuchanganyikiwa na suitofahamu kuhusu jinsi ya kuafikia maagizo hayo.

Kutokuwa na uhakika kuhusiana na kufungwa kwa sehemu za bweni kumeziacha familia zikihangaika kutafuta majibu kuhusu
mustakbali wa elimu ya watoto wao.

Kaunti ya Tana River shule takribani tano ziliathirika na wazazi sasa wakilazimika kuwahamisha watoto wao katika shule nyingine
muhula mpya wa kwanza unapoanza rasmi juma lijalo.

Wazazi kutoka kaunti hiyo ya Tana River wameibua hisia mseto kufuatia agizo la kufungwa kwa shule wakipendekeza serikali
kubadilisha shule hizo kuwa shule za kutwa badala ya kuzifunga ili kuepuka msongamano katika shule nyingine.

Itakumbukwa kuwa Wizara ya Elimu iliangazia tena miongozo yake kufuatia tukio la kutisha la mkasa wa moto wa shule ya

Hillside Endarasha, ambapo watoto 21 wenye umri wa miaka 9 hadi 13 walipoteza maisha.

Masuala muhimu yaliyotolewa na Wizara ya Afya wakati wa tathmini yao ya mabweni ni pamoja na; usalama wa mabweni
Usalama, viwango vya usafi wa mazingira, vifaa vya usalama wa moto na ustawi wa wanafunzi.

Licha ya wasiwasi kutoka kwa wazazi na walimu Wizara ya Elimu inasalia imara, ikisisitiza kwamba shule zote lazima zifuate
kikamilifu viwango hivyo vipya vya usalama.

By Mjomba Rashid