HabariLifestyleNewsSiasa

Afisa Mkuu wa IEBC Avamiwa na Kuuawa na Majambazi Kisauni, Mombasa

Afisa Mkuu wa IEBC ameuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake ni genge la wavamizi wa mapanga.

Imeripotiwa kuwa Aisha Abubakar, Kaimu Mkrugenzi wa IEBC kaunti ya Kilifi alivamiwa nyumbani kwake Utange na genge hilo Jumapili usiku wa manane.

Ripoti ya Polisi imeeleza kuwa washukiwa wawili wa ujambazi waliingia nyumbani kwake Aisha kupitia sehemu ya jikoni walikokata vyuma na kuvamia kwa kumkata kichwani na kumuacha akivuja damu.

Mwanawe Kassim Hassan amejeruhiwa vibaya katika uvamizi huo na sasa akiripotiwa kulazwa hospitali ya Nyali Premier akipokea matibabu.

Majambazi hao walimuibia bidhaa kadhaa zikiwemo simu Samsung A15, Samsung A21, Runinga ya Samsung inchi 65, iPad na bidhaa nyingine za thamani.

Inaarifiwa kuwa Kassim alifanikiwa kumkimbiza mamake hospitalini Nyali alikothibitishwa kuaga dunia.

Kamanda wa Polisi kaunti ya Mombasa Peter Kimani amebaini kuwa maafisa wa Polisi wameanzisha msako mkali wa washukiwa hao wa mauaji.

By Mjomba Rashid