Huduma za matibabu zinatarajiwa kulemaa na kusambaratika kuanzia Jumatatu juma lijalo, pale maafisa wa Kliniki watakapoanza mgomo wao rasmi wa kitaifa.
Kupitia Muungano wao nchini, KUCO maafisa wa afya wameapa kushiriki mgomo kwa madai kuwa serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao, yakiwemo kukamilishwa kwa mkataba wao wa makubaliano, kupandishwa cheo kwa maafisa wa afya kwa mujibu wa makubaliano yao ya awali.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Peterson Wachira maafisa wa afya aidha wamelalamikia serikali kuwaacha nje wauguzi katika mipango ya bima ya afya ya jamii SHA, sasa wakiwataka Wakenya kusaka huduma kwengineko mgomo wao utakapoanza rasmi Jumatatu wiki ijayo.
Maafisa ho wa Kliniki aidha wanamtaka Waziri wa Afya Deborah Barasa, Mkurugenzi wake Mkuu Dkt. Patrick Amoth, Afisa Mkuu Mtendaji na Mwenyekiti wa bima ya afya SHA wajiuzulu mara moja kwa madai ya utepetevu.
Wanasema SHA imewafanya Wakenya kuendelea kutaabika na kuhangaikia matibabu kutokana na kufeli kwa mfumo wa bima hiyo mpya ya afya.
By News Desk