HabariNews

Simameni Imara Kupigania Haki zenu! Uhuru Kenyatta Awasihi Vijana wa Gen Z Kutorejea Nyuma

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta amewahimiza vijana wa Kenya dhidi ya kujitoa katika vita vyao vya demokrasia na utawala bora.

Rais huyo mstaafu amewasihi vijana wa kizazi cha Gen Z waliodaiwa kuanza kuingiwa na hofu hasa kutokana na wimbi la visa vya utekaji nyara, kusimama imara na kutoonyesha hofu katika kushughulikia matatizo ya jamii na kutetea haki zao.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya binamu yake Kibathi Muigai katika Nairobi Chapel mnamo Ijumaa, Kenyatta alisisitiza kuwa haikuwa sawa kwa raia kusalia kimya kwani rasilimali zao hazisimamiwi vyema kutokana na uongozi mbaya unatawala.

Aliendelea kuwasihi wanafamilia wake wachanga pia wajiunge na vuguvugu la vijana wa Gen Z kama njia pekee ya uhakika ya kusimamia wanachokiamini ili kuahkikisha nchi haiangamii mikononi mwa makatili na mafisadi.

Tatizo la watu siku hizi ni kwamba kila mtu anaogopa; sijui mmeogopeshwa, hata wewe Ngina rudi uingie hii. Gen Zs, ninyi ni hadithi ya siku zijazo,” alisema.

“Fight for your rights, sio kukaa hapo mali yenu ichukuliwe na nyinyi mmeitolea jasho! Msikubali, pambaneni muhakikishe mmepata haki yenu, mnaskia? Sio kukaakaa hapo tu. Hakuna kitu kinadumu.”

By Mjomba Rashid