Ubalozi wa Kenya mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni miongoni mwa balazi za kigeni zilizoshambuliwa katika wimbi la machafuko yanayoendelea kushuhudiwa huko.
Ubalozi huo umeshambuliwa katika kile Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing’oei anakiita waandamanaji wavamizi wanaoelezea kutoridhishwa kwao na mzozo katika eneo la mashariki mwa nchi.
Hata hivyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imejitolea kuilipa Kenya fidia kwa uharibifu uliotokana na ubalozi wake mjini Kinshasa baada ya wenyeji kuushambulia na kuupora siku ya Jumanne, huku waasi wa M23 wakiendelea kuukaribia mji mkuu.
Katika taarifa yake Jumanne, Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi alikashifu shambulio hilo la kinyama, akisisitiza kwamba aliwasiliana na mwenzake katika Wizara ya Masuala ya Kigeni nchini DRC kujadili suluhu zinazowezekana.
“Kenya inasikitishwa sana na mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa ofisi za Ubalozi wetu huko Kinshasa, DRC na kundi la watu wenye ghasia wakipinga mzozo mkali Mashariki mwa DRC. Mashambulio hayo yasiyokuwa na msingi, uporaji na uharibifu wa mali pia yameelekezwa kwa ubalozi wa Uganda. Kulikuwa na mipango ya waandamanaji kuvamia, na kushambulia balozi za Afrika Kusini, Marekani na Ubelgiji,” alisema Mudavadi.
Mudavadi anasema kuwa alimweleza wazi Wagner kwamba vitendo hivyo ni ukiukaji wa moja kwa moja wa makubaliano ya kimataifa, na kwamba mamlaka ya DRC lazima ihakikisha ulinzi wa wafanyakazi wa kidiplomasia kwa mujibu wa sheria za kimataifa, hasa Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia.
“Katika majibu ya haraka, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje na Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje na Diaspora amewasiliana na Waziri Mkuu wa DRC, Thérèse Kayikwamba Wagner, ambaye amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kuhakikisha kuwa hatua za haraka zinachukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo. kuweka upya utaratibu.”
Katika wimbi hilo la machafuko watu 17 wameuawa huku mapigano makali kati ya wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na wanajeshi wa serikali ya Kongo yakiendelea kutikisa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mapigano hayo yameacha miili mingi ikitapakaa mitaani, huku hospitali zikitatizika na kulemewa katika kukabiliana na ongezeko la majeruhi.
Rais Félix Tshisekedi alifanya mkutano na viongozi wakuu mjini Kinshasa kujadili mgogoro huo huku waasi wa M23 wakikabiliwa na pingamizi kutoka kwa jeshi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.
Itakumbukwa kuwa Mnamo Jumanne Januari 27, mwaka huu, Rais Tshisekedi aliitisha mkutano na viongozi wa kitaifa huko Kinshasa kushughulikia mzozo unaozidi kuwa mbaya mashariki mwa DRC.
By Mjomba Rashid