AfyaHabariNews

MATAPELI WAMETEKA BIMA YA SHA.

Mwenyekiti wa Kitaifa wa mungano wa wauguzi na matabibu nchini  (KUCO) Dkr Peterson Wachira sasa anadai kwamba  Bima mpya ya matibabu ya SHA imetekwa na Matapeli ambao wanafanya kila juhudi kulemaza utekelezwaji wa Bima hiyo.

Katika mahojiano ya kipekee na Sauti ya Sauti Ya Pwani FM, Dkr Wachira alisema kuwa maafisa ya Kliniki ambao wanafaa kuwa mstari wa mbele katika utekelezwaji wa bima hiyo wametengwa  maksudi na matapeli hao hali ambayo inaashiria ubaguzi na njama ya kutotimiza muktaba wa maafikiano kati ya matabibu na mwajiri wao.

Mwenyekiti huyo wa KUCO alisema kwamba matapeli waliowakuwa katika mfumo wa awali wa Afya wa NHIF, sasa wamehamia katika Bima mpya ya SHA na kwamba ndio wanaolemaza maksudi utekelezwaji wa Bima hiyo nchini.

“SHA haifanyi kazi, wakenya wanalia mahospitalini na ndio maana baadhi wanakataa kujisajili kwa sababu haifanyi kazi. Mahali tumefikia kwa mambo ya SHA sisi kama KUCO hakuna mazungumzo mengine ambayo tunataka.Maafisa wakuu ambao wanafaa kufanikisha utekelezwaji wa Bima hiyo baadhi wameweka maslahi yao mbele.Matapeli  ambao walitatiza mfumo wa NHIF, ndio tu wanaolemaza utekelezwaji wa Bima ya SHA.Tunaomba wachukuliwe hatua za Kisheria.” Alisema Dkr Wachira.

Dr wachira alisema baadhi ya wadau kutoka wizara ya Afya na wengine ambao wametwikwa majukumu ya kuongoza utekelezwaji wa Bima hiyo ya SHA wanalemeza juhudi za kutekeleza bima hiyo  na sasa anataka  wachukuliwe hatua za kisheria mara moja.

Mwenyekiti huyo aidha alidai baadhi ya wadau kutoka sekta ya afya wameweka maslahi yao ya kibinafsi mbele katika bima hiyo hali ambayo inaleta chanagamoto zaidi katika utekelezwaji wake, akimtaka Rais kuwavua majukumu hayo mara moja.

Kauli yangu kwa Rais William Ruto namwambia kwamba wale watu alipea kazi katika wizara ya Afya na pia Bima ya SHA wameshindwa na kazi. Ni vyema wabanduliwe alete watu ambao watahakikisha wakenya wamepata huduma bora za afya kwa mujibu wa kipengee cha 43 cha ibara ya katiba ili tuafikie mpango wa afya kwa wote. Baadhi ya watu wanapaswa kuhakikisha SHA imetekelezwa kikamilifu wana maslahi ya Kibinafsi, watu kama hao hawatatupeleka popote na ndio  wanafanya SHA isifanye kazi.” Alisema Wachira.

Kauli yake Wachira inajiri  baada ya Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki kukiri  kwamba Bima hiyo ya SHA inachangamoto chungu nzima katika utekelezwaji wake, ila serikali kuu na pia serikali za kaunti zinaweka mikakati kabambe kunyoosha hali hiyo ili kufanikisha mpango wa afya kwa wote.

By ISAIAH MUTHENGI