Wanajeshi wa maji wa Japani wameyaomba mataifa ya Afrika kuwa na ushirikiano wa kikanda ili kuimarisha Amani na utangamano.
Kwenye mahojiano na waandishi wa habari mapema leo, kupitia Captain Shinsuke Amano komanda wa wanamaji wa Japan, Japani Maritime Self Defence Force, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano sit u kwa maswala ya kiusalama bali michezo na mazoezi ya kijeshi ya pamoja.
Aidha Bwana Amano ameongeza kusema kuwa meli hizo mbili ambazo walikuja nazo zina uwezo wa kukagua na kutambua vilipuzi vyovyote ndani ya bahari kwa kutumia teknolojia ya Sonar.
Wanajeshi hao wako katika bandari ya Mombasa kwa siku ya pili leo na wanatajiwa kuondoka kesho baada ya kukamilisha muda wa siku tatu humu nchini na kuelekea nchi nyingine huku mwito wao ukiwa ni umoja na amani.
By Editorial Desk