Aliyekuwa mlinzi wa muda mrefu wa Kinara wa ODM Raila Odinga na msaidizi wa kibinafsi George Odiwuor ameaga dunia katika hospitali ya Nairobi West.
Marehemu amekuwa mlinzi wa kibinafsi wa Odinga kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitatu.
Chanzo cha karibu cha familia hiyo ambacho kilitaka hifadhi ya jina kimeripoti kuwa Odiwuor amekuwa akiugua na alikuwa akipokea matibabu katika kituo hicho.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama cha ODM Philp Etale, akitumia ukurasa wake wa Facebook, aliomboleza roho ya marehemu kama rafiki ambaye alisimama naye kwa gharama yoyote.
Tegea taarifa zaidi
Na Mjomba Rashid