HabariNewsSiasa

Ni Mwongo! Justin Muturi Apasua Mbarika na Kupuuzilia mbali Madai ya Utepetevu Aliyolimbikiziwa

Aliyekuwa waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi ameendelea kuikashifiu vikali serikali tawala kwa kushindwa kuwajibikia visa vya utekjeji nyara ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa humu nchini.

Kwenye kikao na waandishi wa habari jijini Nairobi, Muturi ameikashifu serikali kwa kushindwa kuangazia visa hivyo anavyodai vilitekelezwa na maafaisa wa polisi.

Aidha amemlaumu rais Ruto kwa kukosa kujibu barua alizomwandikia kuhusu visa vya utekaji nyara na kuutaja ukimya wake kama ishara kwamba ,masuala ya utekaji nyara hayana umuhimu wowote kwake.

Kwa kuwa sababu zangu za kukosa mikutano ya Baraza la Mawaziri ziko wazi, mtu anaweza kuhitimisha kwamba kuibua wasiwasi kuhusu utekaji nyara na mauaji ya kiholela ni suala nyeti sana kwa Rais,” Muturi akasema.

Wakati uo huo Muturi amekanusha matamshi ya rais kwamba alibanduliwa mamkalani kutokana na kutowajibika kazini akisema kufurushwa kwake kumechangiwa na kuikosoa serikali akimtaja rais kuwa mwongo kwa kauli hizo.

Ni uongo… Sikufutwa kwa sababu ya uzembe na utepetevu, ni kuwa mkweli na kuhoji suala la utekaji nyara

Hadi sasa, Rais hajawahi kuthibitisha kupokea au kujibu barua yangu yoyote kuhusu utekaji nyara na mauaji ya kiholela, Hii inaonyesha wazi kuwa suala hilo sio kipaumbele cha Rais au Baraza la Mawaziri.”

Aidha amedai kuwa washirika wa karibu wa Rais wamekuwa wakimtetea kujiuzulu au kuondolewa kutokana na msimamo wake thabiti kuhusu suala hilo.

Muturi alifichua kwamba alialikwa kwenye mkutano wa mwisho wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Machi 11 katika Ikulu lakini akachagua kimakusudi kutohudhuria.

Na Mjomba Rashid