Kwa mara nyingine tena Jaji Mkuu nchini Martha Koome ametoa hakikisho la kukabiliwa ufisadi vilivyo katika idara ya mahakama.
Jaji mkuu Koome amesisiitiza na kutangaza hatua madhubuti za kupambana na ufisadi katika mahakama zote nchini huku akiwoanya majaji na mahakimu dhidi ya kujihusisha na jinamizi hilo.
Akitoa hutoba yake ya kuangazia masuala ya mahakama na hali halisi ya huduma za mahakama, Koome amesisitiza kuwa hamna ufisadi katika mahakama na kusema kuwa wazo kama hilo halikukuwepo miongoni mwa wafanyakazi wote wa mahakama, japo akikiri kuwa ni tetesi ambazo haziwezi kupuuzwa kwani ni madai makubwa ambayo lazima yaangaziwe vilivyo.
“Ninataka kuangazia na kuzamia katika suala la maadili na ufisadi katika mahakama zetu chini ya huduma ya kupambana na maadili na ufisadi EACC ambapo kuna madai mengi sana ya ufisadi katika mahakama zetu.” Koome alisema.
“Hizi ni tetesi ambazo hatuwezi kupuuza ni madai makubwa ambayo lazima tuangazie na tuchunguze ifaavyo.” Koome alisisitiza.
Koome hata hivyo amewataka majaji na mahakimu kutekeleza wajibu wao jinsi inavyostahiki ili pia kumaliza mrundiko wa kesi mahakamani.
By Mjomba Rashid