HabariMazingiraMombasaNews

Kaunti ya Mombasa Yaihakikishia Familia ya Aliyefunikwa kwenye Jumba Lililobomolewa Kuupata Mwili wa Mpendwa Wao

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imebaini kuwa inafanya kila iwezalo kuopoa mwili wa jamaa aliyefunikwa kwenye vifusi vya jumba la ghorofa 10 lililoporomoshwa.

Hii ni kufuatia lalama za familia kwamba wahusika hawajatoa kipaombele cha kuuondoa mwili kwenye shughuli za uchimbaji na uondoaji wa vifusi hivyo.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, kaunti ya Mombasa imeeleza kusikitishwa na kilichotokea na kwamba inaungana na familia iliyoathiriwa na kisa cha kuporomoka kwa jengo lisilo salama ambapo mpendwa wao Yusuf Ali Abdi ameripotiwa kufunikwa.

Serikali ya Kaunti ya Mombasa iko katika mshikamano wa dhati na familia iliyoathiriwa na kisa cha kuporomoka kilichohusisha jengo lisilo salama katika Barabara ya Abdel Nasser kabla ya Gavana kufanya uamuzi wa kijasiri wa kutekeleza ubomoaji unaodhibitiwa.” Ilisema sehemu ya taraifa.

Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imebaini kuwa imewekeza na kusambaza kila rasilimali inayohitajika ikiemo kutumika kwa mbwa maalum wa kunusa kutoka kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya eneo la Pwani ili kusaidia kuopoa mwili na kuhakikisha familia inaweza kumsitiri mpendwa wao kwa heshima.

Haya yamejiri huku familia ya mfanyabiashara huyo aliyeangukiwa na jumba hilo kwa mara ya kwanza lilipoanza kudidimia mnamo Aprili 2 ikishinikiza kaunti ya Mombasa kuharakisha kuondoa vifusi ili kupata mwili wa mpendwa wao huyo.

“Sisi tumekuwa na subra kama familia na hatujaleta fujo lakini hii iharakishe. Angalia siku 9 saa hizi na hadi kuripuliwa muda huo wote bado kijana yuko pale na ukisikia harufu hiyo sehemu haikaliki.” Akasema mwanafamilia mmoja.

Familia hiyo ilikuwa imetishia kuleta tingatinga wao binafsi kwa kile walichodai kuwa kaunti haijapeana kipaombele kuuondoa mwili huo katika vifusi hivyo.

Itachukua muda gani huyo maiti kutolewa? Kama bindamau si muhimu na wapeana priority kwa chuma kushinda binadamu hiyo haitawezekana.

Hakuna mtu anatusaidia ndugu yetu mwili yake iko pale na hatuna usaidizi mpaka tunataka serika itusaidie.”

Hata hivyo gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassid sasa akibaini kusimama na familia hiyo akiapa kushirikiana nayo kwa kila namna na kupewa msaada ufaao kumpata mpendwa wao huyo.

Hakuna pigo la kumpoteza mpendwa ambayo huwa rahisi – lakini hakuna familia inapaswa kukabiliana nayo bila usaidizi. Gavana yuko pamoja nawe katika wakati huu wa huzuni, na hatapumzika hadi mwisho wa shughuli hii.” Akasema

By Mjomba Rashid