HabariMichezoNews

Wanamichezo Bora Nchini Kutuzwa; Tuzo Za Mwaka Za SOYA Zawadia

Maandalizi yamekamika tayari kwa toleo la 21 la Tuzo za mwanaspoti bora wa mwaka (Soya awards) zitakazoandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa KICC jijini Nairobi 16 Aprili 2025.

Mwenyekiti wa jopo la majaji wa SOYA , Chris Mbaisi amesema timu yake imekuwa mbioni usiku kucha kuhakikisha inachuja uteuzi ipasavyo ili kubaini washindi. Jaji huyu akifichua kwamba zoezi hilo halikuwa rahisi.

“Mwaka wa 2024 ulikuwa na shughuli nyingi kwa wanariadha na wanawake wa Kenya ikiwemo Michezo ya Olimpiki ya Paris na ile ya wanariadha wanoishi na ulemavu bila kusahau kufuzu kwa Junior Starlets kwa Kombe la Dunia la Under-17,” alisema Mbaisi.

Mbaisi alisisistiza kujitolea kwa mwanzilishi wa Soya ambaye pia ni mwanaariadha mashuhuri Paul Tergat kuboresha tuzo hizo kwa kuzindua vitengo vinavyojumuisha mafunzo ya wanariadha katika usimamaizi wa fedha, afya ya akili na uwajibikaji wao katika jamii.

Kauli mbiu ya toleo la 21 la tuzo za Soya itakuwa  “Kuadhimisha ubora wa wanawake katika michezo ” kutokana na matokeo bora yaliyoandikishwa na wanariadha wa kike katika mwaka wa 2024.

Hapo awali kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ilipiga jeki tuzo hizo kwa kutoa hundi ya shilingi milioni moja kama ishara ya kuonyesha kujitolea kwake kuwezesha michezo nchini na kuwaenzi wanaspoti na mashirika ya michezo.

Wanaspoti mbalimbali watatuzwa katika vitengo 11 ikiwemo mwanaspoti bora wa mwaka upande wa wanaume na wanawake,mwanaspoti bora kwa wanariadha wanaioshi na ulemavu,kocha bora wa mwaka, timu bora ya mwaka kwa wanawake na pia wananume ,shule bora ya wavulana na wasichana , kocha bora wa mwaka wa shule na hata ukumbi wa umaarufu, (hall of fame).

Bingwa mara mbili wa Mbio za Olimpiki Beatrice Chebet,bingwa mara tatu wa mbio za mita 1,500 ambye pia ni mshilkilizi wa rekodi ya dunia katika mbio hizo Faith Kipyegon na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za wanawake Ruth Chepng’etich watashindania  tuzo ya Mwanaspoti Bora wa kike  Mwaka wa 2024.

 

Wakati uo huo , bingwa wa Olimpiki wa mita 800 Emmanuel Wanyonyi, bingwa wa ndondi wa uzani wa light middleweight Boniface Mugunde na mshindi wa medali ya fedha ya Olympic mita 5,000 Ronald Kwemoi ni miongoni mwa walioteuliwa kuwania tuzo ya wanaume.

 

Naye mshindi wa medali ya fedha kwenye mbio ndefu za wanariadha wanaoishi na ulemavu Samson Ojuka na mshindi mara mbili wa medali ya dhahabu katika Michezo ya Vijana ya Dunia Michelle Chepng’etich ni miongoni mwa walioteuliwa kuwania tuzo za Mwanaspoti na mwanamke mwenye Ulemavu mtawalia.

Mwanaspoti bora wa Mwaka, wanawake :

Imani Cherotich

Ruth Chepngetich

Beatrice Chebet

Hellen Obiri

Faith Kipyegon

 

Mwanaspoti Bora wa Mwaka,wanaume :

Boniface Mugunde

Albert Odero

Benson Kipruto

Emmanuel Wanyonyi

Ronald Kwemoi

 

Kocha Bora wa Mwaka:

Abdallah Otieno

Beldin Ademba

Kevin Wambua

Salim Babu

Mildred Cheche

 

Mwanaspoti bora kwa wanawake wanaoishi na ulemavu:

Sheila Wanyonyi

Caroline Wanjira

Rehema Anjenjo

Michelle Chepngetich

Valery Olesia

 

Mwanaspoti bora kwa wanaume wanoishi na ulemavu:

Samson Ojuka

Kennedy Ogada

Shadrack Kipyegon Mutai

Dedan Ireri Maina

Dennis Cheruiyot

 

Timu bora ya Wanawake:

Kenya women’s amputee national team

Kenya Pipeline

Malkia Strikers

Junior Starlets

Police Bullets

 

Timu bora ya wanaume:

Kenya Prisons (Voliboli)

Nairobi Thunder

Rising Stars

Shujaa

Kabras Sugar

 

Timu bora ya Shule ya wavulana :

All Saints Embu (Raga ya 15s)

Friends School Kamusinga

Shule ya Upili ya Wavulana ya Musingu

Shule ya Upili ya Vihiga

St Charles Lwanga

 

Timu bora ya Shule ya wasichana :

Shule ya Sekondari ya Kesogon

Shule ya Upili ya Wasichana ya St Joseph Kitale

Shule ya wasichana ya  Butere

Shule ya wasichana ya Tigoi Girls

Shule ya Upili ya Wasichana ya Kinale.

 

By Mohammed Mwajuba