Rais William Ruto ameagiza Wizara ya Leba kwa ushirikiano na wizara ya utumishi wa umma kufanikisha nyongeza ya mishahara ya asilimia 6 kwa wafanyakazi wake.
Rais amekemea hatua ya waajiri kushindwa kutekeleza nyongeza hiyo ya mishahara licha ya kuafikiwa hilo mwaka ule 2023.
Ameleeza kuwa si vyema wafanyakazi kukosa nyongeza hiyo na kwamba kamwe hilo halitakubalika chini ya uongozi wake.
“Haikubaliki kwa waajiri kutotekeleza nyongeza ya kima cha chini cha mishahara. Wizara ya Leba inapaswa kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa,” alisema Rais Ruto.
Rais Ruto aidha ametangaza kuwa malipo ya uzeeni na tozo kwa wafanyikazi katika sekta ya kibinafsi na ya umma hayatakatwa ushuru kuanzia mwaka ujao wa kifedha.
Hatua hii ya mageuzi Rais alieleza, inapendekezwa katika Mswada wa Fedha wa 2025 kwa kutambua huduma na kujitolea kwa wafanyakazi katika miaka yao ya kazi, na hatua ya kuhakikisha kuwa wanastaafu kwa heshima.
By Mjomba Rashid