Waliotekwa nyara kufuatia maandamano ya kupinga mswada tata wa fedha wa mwaka 2024 waliachiliwa na kurejeshwa kwa familia zao.
Ni kauli yake Rais William Ruto, akizungumza katika Ikulu ya Nairobi wakati wa mahojiano na wanahabari kwenye ziara ya rais wa Finland, Alexander Stubb.
Rais Ruto ameshikilia kwamba amesimama na ahadi yake aliyotoa kwa Wakenya wakati wa kampeini kwamba hataruhusu visa vya utekaji nyara na serikali yake haitahusika kivyovyote.
Aidha Ruto amedokeza kuwa serikali ya Kenya ni taifa la kidemokrasia na hakuna visa vya utekaji nyara vitakavyoshuhudiwa katika serikali yake ya Kenya Kwanza.
“Wote waliotekwa au kupotea wamepelekwa nyumbani kwao na nimeelekeza kwa uwazi kabisa kwamba jambo kama hilo halitarudiwa tena nchini Kenya.”
Wakati uo huo kiongozi huyo wa taifa ameeleza kuwa maswala yanayohusisha polisi humu nchini sasa yako chini ya Wakuu wa idara ya polisi hasa Inspoekta Jenari wa polisi ili kupeana nafasi hiyo ya kuweza kujitegemea katika idara hiyo pasi na kuingiliwa majukumu yake.
By News Desk