Serikali imepuuzilia mbali madai ya upinzani kuzuiwa kuingia nchini Tanzania, baada ya Wakili na Kiongozi na chama cha PLP Martha Karua na wenziwe kuzuiwa na kufurushwa nchini Tanzania.
Katika taarifa yake Jumatatu Msemaji wa serikali Dkt. Isaac Mwaura alisema kunyimwa ruhusa kuingia Tanzania hakuhusiani na jukumu la Karua kama mwanachama wa upinzani nchini Kenya.
“Kama serikali fulani inahisi kama ina taarifa kuhusu mtu fulani, iwe serikalini au upinzani, ina haki ya kufanya hivyo na kukiri. Sio suala la upande gani wa mgawanyiko wa kisiasa,” alisema Mwaura.
Akizungumzia kufukuzwa kwa wakili Martha Karua na serikali ya Tanzania, Mwaura amekana kuhusishwa suala hilo na siasa za upinzani akisema ni uamuzi wa serikali yenyewe ya Tanzania ambao hauwezi kuingiliwa.
Msemaji huyo amedokeza kuwa viongozi wengine wa upinzani wamesafiri kwa uhuru, na kuthibitisha kuwa hakuna serikali kuingilia kati harakati za kisiasa.
“Wakati Raila Odinga alipokuwa kiongozi wa upinzani, alikuwa akisafiri sana hadi Tanzania,” akaongeza.
Pia amebaini kuwa uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania bado upo imara akieleza kuwa kufukuzwa kwa Martha Karua ni uamuzi uhuru wa Tanzania tu, na haukuchochewa kisiasa.
“Hakuna malumbano ya kidiplomasia kati ya Kenya na Tanzania. Nchi yoyote ina haki ya kukaribisha mtu yeyote ndani ya maeneo yake,” akasema.
Wakati uo hio Mwaura amepuuzilia mbali madai ya propaganda na dhulma za kisiasa kwa kukamatwa kwa hivi majuzi kwa Mbunge Mumias Mashariki Peter Salasya, kunatokana na mienendo ya mtu binafsi, na sio misimamo ya kisiasa.
By Mjomba Rashid